24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza ‘kusubiri’ makubaliano na Marekani

RAIS Barack Obama
RAIS Barack Obama

HANGZHOU, CHINA

RAIS Barack Obama amesisitiza Uingereza ‘itasubiri’ kufanya makubaliano ya kibiashara na Marekani huku akionya hatua zinahitajika kuzuia mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (EU) kuharibu uhusiano maalumu baina ya mataifa hayo.

Rais huyo wa Marekani alisababisha ghadhabu nchini Uingereza wakati wa kampeni ya kura ya maoni miezi minne iliyopita kuhusu taifa hilo kubaki au kujiondoa kutoka EU.

Alikaririwa akisema Uingereza itarudi kusimama ‘nyuma ya foleni’ kusubiri kuingia makubaliano iwapo itaamua kujiondoa kutoka umoja huo.

Kauli hiyo aliyoitoa wakati wa mkutano wa pamoja na wanahabari na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Aprili mwaka huu ililaaniwa vikali ikihesabiwa kama uingiliaji wa siasa za ndani za taifa hilo.

Na kura za maoni ziliiona ililenga kuwatisha wapiga kura.

Lakini alipoulizwa kuhusu kauli yake hiyo wakati akihudhuria mkutano wa mataifa 20 tajiri na yanayokuja juu kiuchumi (G20) jana, Obama, ambaye anaondoka madarakani Januari mwaka ujao alikataa kuifuta na alienda mbali zaidi kuonya suala hilo linatishia uhusiano maalumu baina ya mataifa hayo.

Wakati akisisitiza kuwa hakuwahi kusema Uingereza itaadhibiwa kwa kupiga kura ya kujiondoa EU, Obama alirudia mtazamo wake kuwa ‘dunia ilinufaika zaidi na uwapo wa Uingereza ndani ya EU’.

Na aliweka wazi majadiliano mapya ya kibiashara yanayoendelea na EU yatabakia kipaumbele cha Marekani licha ya uwapo changamoto.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jijini hapa, ambako mkutano wa kilele wa G20 unafanyika, Obama alisema: ‘Majadiliano hayo yanaendelea.

Wote Obama na May walisema watajaribu kupunguza athari za kujitoa kwa Uingereza EU kwa uhusiano wao maalumu.

Katika picha ya pamoja ya viongozi wa G20 jana, May alikaa mstali wa katikati kati ya mitatu ya viongozi hao huku wenzake wa
mataifa saba tajiri (G7) wakikaa mstali wa mbele. Kwa mmujibu ya wachambuzi wa mambo, kitendo hicho kinaonesha kuelekea kutimia kwa utabiri wa Obama kuhusu kushuka kwa hadhi ya Uingereza ikijiondoa EU.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles