28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

UHUSIANO WA KIMAPENZI UNAVYOWEZA KUANZISHWA BILA KUTARAJIWA

Na CHRISTIAN BWAYA,

UNAWEZA kushangaa lakini ndio ukweli wenyewe kwamba upo uwezekano mkubwa wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na mtu yeyote bila kujali mwonekano wake, tabia wala imani yake.

Katika makala haya tunaeleza kanuni za kimaumbile zinazoongoza uhusiano wa watu wawili ambao mara nyingi hukutana kwa njia ya nasibu.
Pamoja na imani kwamba uhusiano bora unawezekana kwa kukutana na mtu sahihi, wataalamu wa masuala ya uhusiano wanasema mwanamke yeyote anaweza kuwa na uhusiano na mwanamume yeyote.
Hata hivyo, kuna mambo matatu muhimu yanayoweza kuanzisha uhusiano ambayo ni:

Hisia za kimapenzi au tamaa  Ingawa tamaa ina nguvu kubwa katika kuanzisha uhusiano, si rahisi kudumu kwa muda mrefu. Misingi ya hisia hizi za kimapenzi ni maumbile yanayoonekana.

Urafiki au ukaribu unaojenga Mazingira ya watu wawili kuwa karibu kihisia. Misingi ya ukaribu huu ni namna gani mahitaji ya kihisia ya mwenzi yanavyotambuliwa na kujibiwa bila kujali urafiki huo umetokana na tamaa au uamuzi.

Kuweka ahadi

Ingawa kwa watu wengi dhamira ya kudumisha uhusiano hutokana na ahadi za awali, wakati mwingine, hutokea uamuzi huo ukawa chanzo cha kuchipua urafiki na hisia kama ilivyokuwa kwa wazee wetu zamani. Hiki ndicho kiwango cha juu cha uhusiano.
Sasa, ingawa uhusiano unaweza kuchipukia kokote kati ya tamaa, urafiki na uamuzi kutegemeana na imani, mitazamo na utamaduni wa wahusika, kilicho muhimu zaidi ni kile kinachofanyika baada ya uhusiano huo kuanzishwa ili kuufanya uendelee.

Uhusiano unavyoanza
Kwa kawaida, uhusiano huanza pale mtu anapovutiwa na mwingine iwe kihisia au kimwili. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza kabisa ambayo hutegemea masuala makuu mawili.

Kwanza kabisa ni ukaribu, inasemekana kwamba, watu wawili wanapojikuta bila hata wao wenyewe kutarajia katika mazingira ya ukaribu iwe kwa kufanya kazi ofisi moja, kuabudu mahali pamoja, kusoma au kuishi mtaa mmoja, huongeza uwezekano wa mmoja wao kuvutiwa na mwenzake na hivyo kuanzisha uhusiano.
Tafiti zinathibitisha kwamba kadri unavyokutana na mtu iwe kwa kumwona na kumsikia mara kwa mara, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kumpenda na kwamba kwa kawaida watu huwa hawavutiwi na vitu wasivyovijua kwa karibu. Kwa maana nyingine, kadri unavyokutana na mtu ndivyo unavyojikuta ukizidi kumpenda.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles