22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

UHUSIANO WA KIMAPENZI KWA WALIMU, WANAFUNZI CHANZO CHA MATOKEO MABAYA

Tabia ya baadhi ya walimu kujenga uhusiano ya kimapenzi na wanafunzi husababisha matokeo mabaya katika masomo yao.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumanne Februari 21, mjini Dodoma katika mkutano wa wadau mbalimbali wa elimu akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wabunge, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine. 

 

Kamanda Muroto amesema tabia hiyo ya baadhi ya walimu kuwa na uhusiano wa mapenzi na wanafunzi wao imekithiri na hivyo kusababisha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi pamoja na mmomonyoko wa maadili. 

“Baadhi ya walimu wamekuwa na tabia mbaya za kutembea na wanafunzi, hivi unakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi halafu baadaye darasani ukiwa unamfundisha ataelewa kweli, hivyo baadhi ya walimu wenye tabia hii wanachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kushika nafasi za mwisho,” amesema Muroto.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Deogratus Ndejembi amesema mojawapo ya mkakati wao ni kusoma matokeo ya wanafunzi katika mikutano ya hadhara ili kila mwananchi ajue matokeo ya mtoto wa jirani yake ambapo itaongeza chachu ya wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma pia italeta hamasa kwa wanafunzi kujisomea zaidi.

 

“Sababu nyingi zinajirudia kama walivyoziainisha wakuu wa wilaya wenzangu, ila katika wilaya yangu tuna mikakati mingi tuliojiwekea ikiwamo kusoma matokeo ya wanafunzi katika mikutano ya hadhara ili kuwapa hamasa wazazi na wanafunzi,” amesema Ndejembi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles