32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Uhuru wa uhariri unaingiliwa – Wakili Marenga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

HATUA ya mhariri wa chombo cha habari kuelekezwa na serikali taarifa za kuchapisha, kama ilivyolekezwa na kifungu cha cha 7 (2) (b) cha sheria hiyo, inaingilia moja kwa moja uhuru wa mhariri katika kutoa ama kuchapisha habari.

Wakili James Marenga akifafanua jambo kwenye semina hiyo.

Akizungumza kwenye semina na wanahabari, James Marenga ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Makamu Mwenyekiti wa MISA – TAN ameeleza kuwa, kifungu hicho cha sheria kinapoka mamlaka ya mhariri katika kuamua habari gani ya kuchapishwa.

“Kifungu cha 7 (2) (b) (iv) cha Sheria ya Huduma za Habari, kinatoa maelekezo kwa vyombo vya habari binafsi kuchapisha habari zenye umuhimu kwa taifa kwa maelekezo ya Serikali.

Kifungu hiki cha Sheria kinaingilia uhuru wa uhariri na hasa kwenye vyombo vya habari vya binafsi. Kifungu hiki kidogo hakiwezi kufanyiwa marekebisho, tunapendekeza kifutwe,” amesema.

Amesema, mapendekezo yanakusudia kuwezesha maamuzi ya kihariri kuzingatia vigezo vya taaluma bila kuathiriwa na maamrisho yasiyo ya kitaaluma. Uhuru wa uhariri (editorial independence) utalindwa.

Akifafanua zaidi amesema, kifungu cha 7 (3), (a), (b), (c), (f), (g), (h), (i) na (j) vya Sheria hiyo, vinatoa udhibiti wa aina fulani ya habari ama maudhui.

“Mamlaka hii ya kisheria inatoa mwanya kwa serikali kudhibiti taarifa zinazotolewa na vyombo binafsi vya habari.

“Kifungu hiki na vifungu vyake vidogo vinakiuka uhuru wa wa kujieleza bila ya kuwa na sababu za msingi. Hii pia ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ).

Amesema, tunapendekeza kifungu hiki na vifungu vyake vidogo vifutwe kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki. (EACJ),” amesema Wakili Marenga.

Kwenye semina hiyo Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, wameungana kwa pamoja katika kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki kwa wanahabari kufanya kazi zao.

“Kuna sheria nyingi zilizowekwa na kulenga waandishi ama kushambulia tasnia, kwa tumeungana kwa pamoja kuhakikisha sheria hizo zinaondolewa makali yanayoumiuza wanahabari.

“Ni bahati nzuri sasa serikali nayo imeliona hili, mwelekeo wetu ua matumaini lakini tunapaswa kuendelea pamoja mpaka tunafikia lengo,” amesema Balile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles