23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

‘UHURU WA PALESTINA NI UFUNGUO WA AMANI MASHARIKI YA KATI’

BETHLEHEM, UKINGO WA MAGHARIBI


RAIS Mahmud Abbas wa Palestina amesema kupatikana kwa uhuru wa taifa lake ndio ufunguo wa amani na utulivu katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Ameyasema hayo mjini hapa juzi, alipokuwa na mkutano wa pamoja na mgeni wake, Rais Donald Trump wa Marekani.

Abbas alisisitiza kuwa matakwa ya wafungwa wa Kipalestina walio katika jela za Israel ni ya haki na ni wajibu wa taifa hilo kuyatekeleza.

Aidha alitilia mkazo dhamira yake ya kushirikiana na Trump katika kufanikisha mpango wa amani wa kihistoria na Waisraeli.

Mkuu huyo wa taifa la Palestina, alisisitiza msimamo wa Palestina unaotegemea utatuzi kwa uwepo wa dola mbili chini ya mkataba wa mipaka wa mwaka 1967.

Mkataba huo unataja dola la Palestina ikiwa na mji mkuu wake Jerusalem ya Mashariki na dola ya pili ni Israel.

Rais Abbas alifafanua kuwa mzozo uliopo eneo hilo si wa kidini kwa kuwa kuheshimu dini zote na mitume wake ni sehemu ya imani ya taifa la Palestina na kusisitiza kuwa tatizo lililopo ni uvamizi, ujenzi wa makazi ya walowezi na kutokubali kwa Israel juu ya uwepo wa dola ya Palestina.

Kwa upande mwingine, Rais Abbas amelaani vikali shambulio baya la kigaidi, lililotokea hivi karibuni mjini Manchester, Uingereza lililosababisha vifo vya watu 22 na kujeruhi wengine wengi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,319FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles