26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

UHURU: NASA INAWATAFUTIA VIONGOZI WAKE AJIRA

NAIROBI, KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta ameusuta ushirika wa upinzani wa NASA akisema ajenda na sera zake zimeegemea  kuwatafutia vigogo wake ajira badala ya vijana.

Matamshi ya Rais Kenyatta yamelenga uzinduzi wa muongozo wa hivi karibuni wa NASA, ambao Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga aliteuliwa kupeperusha bendera ya NASA huku wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka akiteuliwa kuwa naibu wake.

Wengine Musalia Mudavadi wa Chama cha ANC akiteuliwa kuwa Waziri Mkuu akisaidiwa na manaibu, Moses Wetangula wa Chama cha Ford-Kenya na Gavana Isaac Rutto wa  CCM.

Kwa sababu hiyo, Rais Kenyatta alisema muongozo huo mpya wa uongozi wa NASA umelenga kuwatafutia vinara hao kazi badala ya kujikita kwa vijana.

“Sisi tunawatafutia vijana wote kazi si kama hawa wenzetu wanaowatafutia viongozi wanne,” alisema Rais Kenyatta kwenye Uwanja wa Kasarani wakati wa kongamano la chama cha KANU la kuunga mkono Serikali ya Jubilee kuchaguliwa tena Agosti 8 chini ya mgombea urais, Rais Kenyatta.

“Tunajali maslahi ya vijana kwa kuwatafutia kazi. Nikirejea matamshi ya Rais Mstaafu Daniel Arap Moi, tunataka upendo, amani na umoja nchini," aliongeza Rais Kenyatta.

Aidha Rais Kenyatta alisema wananchi wapewe fursa na nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani.

“Tukifanya hivyo Mungu atatubariki kwa amani. Tunaomba muwe mstari wa mbele tuhubiri amani," alisema Rais Kenyatta.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,371FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles