23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Uhuru Mchanganyiko yajivunia mafanikio kitaaluma

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko imetimiza miaka 100 tangu ilipoanzishwa mwaka 1921 huku ikijivunia kufanya vema katika ngazi ya taaluma.

Shule hiyo yenye wanafunzi 584 inajumuisha watoto wasio na ulemavu na wenye ulemavu ambao ni wasioona, wenye ualbino, viziwi na ulemavu wa akili.

Akizungumza wakati wa mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Christina Wambura, amesema imekuwa ikipata mafanikio makubwa kitaaluma, kimazingira na kimichezo.

Kwa mujibu wa mwalimu Wambura kwa miaka minne mfululizo 2017, 2018, 2019 na 2020 shule imefaulisha wanafunzi wote wa darasa la saba huku na kushika nafasi ya kwanza kikata.

Mkuu wa Mauzo wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Tumaini Alila, akipata maelezo kutoka kwa wahitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kuhusu masuala mbalimbali waliyojifunza. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Wambura.

“Mafanikio haya yote ni mazao ya uongozi bora wa shule na ushirikiano mzuri wa walimu, wazazi na wafanyakazi wasio walimu pamoja na kamati ya shule wanaohakikisha inazidi kusonga mbele,” amesema Mwalimu Wambura.

Hata hivyo amesema wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa madawati 60 na kati ya hayo 50 ni ya kawaida na 10 ni kwa ajili ya darasa la kwanza wasioona.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkuu wa Mauzo wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Tumaini Alila, amesema wataendeleza ushirikiano wao na shule hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili.

“Tumepokea baadhi ya maombi hasa mahitaji muhimu ya shule tumeyachukua ili kuona ni namna gani tunaweza tukasaidia,” amesema Alila.

Katika mahafali hayo baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika ngazi mbalimbali walizawadiwa vyeti vya pongezi huku wenye ulemavu wakiwapiku wenzao kwa kupata zawadi za taaluma, usafi na michezo.

Mwanafunzi asiyeona akighani shairi la kuwaaga wahitimu wakati wa mahafali ya darasa la saba Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. Umahiri wake uliwashangaza wengi na baadhi ya wageni waalikwa walishindwa kujizuia na kutoa machozi.

Mmoja wa wahitimu Maua Rashidi ambaye ni kiziwi mwenye uoni hafifu amesema matarajio yake ni kuja kuwa daktari kwa sababu anapenda masomo ya sayansi.

Aidha katika sherehe hizo mwanafunzi asiyeoona ambaye alighani shairi la kuwaaga wahitimu aliwaliza wageni waalikwa kutokana na umahiri aliokuwa nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles