Amsterdam, Uholanzi
Serikali ya Uholanzi imesema imesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 mpaka angalau tarehe 29 mwezi huu wa Machi kama hatua ya tahadhari.
Serikali imesema hatau hiyo inayofuatia uamuzi kama huo uliochukuliwa na Ireland mapema jana, unatokana na ripoti kutoka nchini Denmark na Norway za uwezekano wa kusababisha athari.
Mamlaka za afya za Norway zilisema siku ya Jumamosi kuwa maafisa wake watatu waliodungwa chanjo hiyo walikuwa wakitibiwa hospitalini kwa kuvuja damu, damu kuganda na kiwango cha chini cha chembechembe za damu.