23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uhamiaji yatoa hati mpya za kusafiria 321,117

LEONARD MANG’OHA – DAR ES SALAAM

IDARA ya Uhamiaji imetoa zaidi ya hati 321,117 za kusafiria za kielektroniki zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.8 tangu kuzinduliwa kwa hati hizo Januari 31 nwaka 2018.

Akizungumza jana katika mahoajino maalumu na MTANZANIA Dar es Salaam, Mrakibu Mwanamizi wa Uhamiaji na Msemaji wa idara hiyo, Ally Mtanda, alisema kuwa hati hizo ni pamoja na 318,656 za kawaida, 524 za utumishi, 1932 za kidiplomasia na hati maalumu tano za kidiplomasia ambazo hutolewa kwa viongozi wakuu wa nchi.

Mtanda alisema kuwa utoaji wa hati hizo kwa njia ya kielektroniki umerahisisha utendaji wa idara hiyo na kupunguza muda wa mteja kupata hati sasa mtu anaweza kuwasilisha maombi na kupata hati hiyo siku inayofuata.

Kuhusu utoaji wa vibali vya ukaazi alisema kuwa kwa sasa idara hiyo inavitoa kwa haraka na bila usumbufu wowote hasa baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji wa vibali hivyo kielektroniki Novemba mwaka 2018 ambao huimwezesha mtu kuomba vibali hivyo akiwa popote duniani.

“Jumla ya vibali vya ukaazi vilivyotolewa daraja A vinavyotolewa mwa wawekezaji ni 560, daraja B vinavyotolewa kwa waajiriwa wa fani mbalimbali ni 3741 na daraja C ambavyo hutolewa kwa wageni ambao si wawekezaji wala waajiriwa ni vibali 1,170,” alisema Mtanda.

Kuhusu baadhi ya waombaji kushindwa kuchukua hati zao hata baada ya kukamilishwa alisema kuwa jambo hilo linatokana na baadhi yao kutokuwa na malengo ya safari.

Mtanda alisema kuwa moja ya masharti ya kupewa hati mpya ni pamoja na kumtaka mwombaji kuwasilisha hati yake ya zamani hivyo wale ambao hawajachukua hati hizo hawatapewa hati nyingine hadi hapo watakapowasilisha zile za zamani.

Alisema kuwa licha ya kuwa pasipoti ni hati ya kusafiria pia ni nyaraka ya kiusalama hivyo ni lazima idhibitiwe kwa sababu unaweza kutumika vibaya hasa wakati huu ambapo kumekuwa na wimbi la biashara haramu ya dawa za kulevya na ugaidi.

Kuhusu kuwapo malalamiko ya baadhi ya watu kulalamikia kunyimba hati hizo kwa madai ya kuwa si raia wa Tanzania alisemna kuwa kadhia hiyo imekuwa ikiwakumba baadhi ya raia ambao wazazi wao wote si Watanzania ambapo awali sheria ilikuwa ikiwatambua kwa kuzaliwa kwao tu hapa nchini tofauti na sasa ambapo sheria inataka mzazi mmoja awe raia wa Tanzania.

Kuhusu kukamakwa kwa raia wa kigeni wakiwa wanafanya kazi bila kuwa vibali alisema kuwa wengi wao huingia nchini lakini baada ya vibali vyao kuisha husundwa kuomba vingine au huchelewa kupata vibali vya kazi kutoka katika mamlaka husika hivyo wanapokamatwa uhesabiwa kama wahamiaji haramu.

Aidha aliwataka madereva wanaofanya kazi zao katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuomba hati za kusafiria badala ya kuchukua vibali vya muda mfupi ambavyo ni ghali kutokana na kutumika mara moja.

Mtanda alisema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa madereva hao wameamua kuwakuanzisha dirisha maalumu la kuwahudumia ili kuwawezesha kuvipata haraka.

Alisema tayari idara hiyo imewatambua jumla ya wahamiaji 1,300 wa Ethiopia katika magereza mbalimbali nchini ambapo kati yao 869 wamerejeshwa nchini mwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles