23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

UHAMIAJI WAZITIKISA SIMBA, YANGA, AZAM

makocha-wa-vpl

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

IDARA ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam, imezipiga marufuku klabu za Simba, Yanga na Azam FC kuwatumia makocha na wachezaji  wa kigeni katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara hadi watakapokamilisha maombi ya vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Klabu hizo zinadaiwa kuwatumia wachezaji na makocha hao wa kigeni bila kuwa na vibali vya kufanya kazi wala kuishi huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi.

Simba imetajwa kuongoza kuwa na wachezaji wengi wasiokuwa na vibali vya kuishi wala kufanya kazi akiwamo kipa, Daniel Agyei, James Kotei, Laudit Mavugo, Mussa Ndusha, Javier Bukungu na Fredrick Blagnon.

Klabu hiyo pia imetajwa kuwatumia makocha wake, Joseph Omog, Jackson Mayanja na kocha wa makipa, Iddi Salim kutoka Kenya bila ya kufuata utaratibu.

Yanga wamekamilisha taratibu hizo kwa asilimia 70 huku wakituhumiwa kuwatumia makocha wake, George Lwandamina, Noel Mwandila na kiungo, Justine Zulu ambao hawana vibali vya kuishi wala kufanya kazi nchini.

Tuhuma hizo pia ziliwagusa Azam kwa kuwatumia wageni 13 akiwamo beki Yakubu Mohammed, washambuliaji; Yahaya Mohammed, Daniel Amouah, Samuel Afful, Enock Agyei, wote kutoka Ghana na kiungo mkabaji, Stephan Kingue Mpondo kutoka Cameroon.

Mbali na wachezaji hao, pia Idara hiyo iliwataja makocha watano ambao ni Zeben Hernandez, Yeray Romero, Jose Garcia, Sergio Perez na Joseph Nzawila pamoja na wafanyakazi wawili wa kigeni ambao hawana vibali vya kuishi wala kufanya kazi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, John Msumule, alisema kuwa kwa klabu itakayokiuka agizo hilo  itachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe  fundisho kwa klabu nyingine zenye kuvunja sheria za nchi.

“Tumechukua uamuzi huu baada ya kufanya uchunguzi na kuwahoji viongozi wa klabu husika kutokana na kuvunja sheria za nchi.

“Viongozi wa Azam walisema kuwa vibali wanavyo na wanavileta leo (jana), hivyo tunawasubiri hata hivyo walisema watavileta kabla si kusubiri kufuatwa,” alisema Msumule.

Msumule alisema kuwa operesheni hiyo ya ukaguzi wa vibali itakuwa ni mwendelezo ili kuhakikisha klabu zote za soka nchini zinafuata sheria na taratibu za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles