24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uhamiaji, TRA Kagera watakiwa kutoa elimu

Na Renatha Kipaka, Kagera

Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) mkoani Kagera wametakiwa kutokuwa vikwazo kwa wafanyabiashara wanaotoka nchi jirani zilizopo katika Jumuhiya ya Afrika Mashariki na kuanza utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyiashara hao ili kuondoa vikwazo wanavyokumbana navyo mipakani.

Mkurugenzi Kampuni ya Utalii, William Rutta.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Toba Nguvila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika ufunguzi wa maonyesho ya kwanza ya Kibiashara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika uwanja va CCM Katika, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Hayo yamejiri kufuatia maelezo ya Mratibu wa Maonyesho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii, William Rutta katika taarifa iliyobainisha kuwepo kwa vikwazo ikiwemo vizuizi mbalimbali mipakani kwa wafanyabiashara.

Aidha, Nguvila amesemtaka Meneja wa TRA Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera kuanza mara moja utaratibu wa kuelimisha wafanyabiashara ili kuwapunguzia vikwazo wanavyovipata.

“Nitumie nafasi hii kuwaelekeza Idara ya Uhamiaji na ile ya TRA kutoa elimu na kupokea changamoto ili kupunguza vikwazo, kuanzia sasa wekeni banda katika maonyesho haya najua kuna changamoto ambazo wafanyabiashara wa nje wamezipata wakati wakija mkoani hapa ikiwemo vizuizi,” amesema Nguvila.

Ameongeza kuwa siyo vyema viongozi kuwa vikwazo, bali wawe fursa ya kuwawezesha wafanyabiashara kufanikiwa zaidi.

Aidha amekemea vikari Rushwa mipakani , tozo zisizo na maana, badala yake vitumike vibali vya kisheria ambavyo haviwaletei madhara wala kuwakwamisha wafanya biashara.

Nae, Mratibu wa maonyesho hayo, William Rutta amesema iwapo vikwazo vikiondolewa wafanyabiashara watafanya biashara zao kuwa uhuru zaidi.

Amesema lengo la maonyesho hayo ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu ambaye amefungua milango ya nchi kwa kuleta wageni tofauti tofauti wenye kutalii na kufanya biashara ikiwamo kuwezesha mkoa huo kujinasua katika namba mbaya kiuchumi.

Hata hivyo, mratibu huyo amesema kuwa hadi sasa tayari wafanya biashara kutoka nchi za Burundi, Kongo DR, Kenya, Uganda na Rwanda tayari wako mkoani Kagera.

Maonyesho hayo yaliyoanza Juni 15, yalifunguliwa rasmi Juni 25, na yatafungwa Julai 10, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles