25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Uhamiaji Kagera yawarejesha makwao watoto 543

Na Renatha Kipaka, Kagera

Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera imesema jumla ya watoto 543 ambao ni wahamiaji walirejeshwa kwenye nchi zao mwaka 2021 baada ya kukamatwa umla ya watoto 543 walikamatwa na kurejeshwa nchini kwao kutokana na kuishi mkoani Kagera bila kibali.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Thomas Fussy, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Amesema watoto hao na idadi yao kwenye mabano ni kutoka nchi sita zinazopakana na mkoa wa Kagera ambazo ni Burundi(402), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(2), Rwanda(86), Uganda(51), Zambia(1) na Ethiopia(1).

Fussy amesema kuwa mafanikio hayo ya kuwakamata wahamiaji hao yanatokana na msako ambao umekuwa ukifanyika chini ya maofisa wa idara ya uhamiaji kwenye wilaya zote zinazopakana na nchi hizo jirani.

“Iwapo watendaji wa mitaa na vijiji watafikisha elimu kupitia mikutano inayofanyika kwa wananchi itaongeza uimarishaji wa ulinzi kwa kuwafichua wanaoishi kinyume na taratibu,” amesema.

Amesema, wahamiajai huingia nchini kupitia njia mbalimbali zisizo halali na kufanya makazi katika vijiji na vitongoji ndani ya mkoa na kuanza kushiriki shughuli zinazofanywa na wazawa.

Aidha amesema kuwa watoto hao wamekuwa wakifanyishwa shughuli za vibarua kwenye mashamba ikiwamo pia kuchunga mifugo.

“Ukimkamata wilaya ya Biharamulo anakwambia ameingilia wilaya ya Misenyi lakini anachokifanya huko ni kuchunga ng’ombe wa mtu na sio kwamba atakaa hapo anaenda mbali zaidi jambo ambalo kiusalama siyo zuri,”mesema Fussy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles