22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

UHABA WA WAKUNGA DUNIANI KUFIKIA MILIONI 14 AFRIKA 2030

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mabara ya Asia na Afrika yatakabiliwa na uhaba mkubwa wa wakunga wataalamu ifikapo 2030 ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa, imeelezwa.

Uhaba uliopo sasa ni kiwango cha milioni tisa ifikapo 2030 ambapo utaongezeka hadi kufikia milioni 14.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA – Tanzania), Jaquiline Mahon alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo hapa nchini yatafanyika mkoani Morogoro.

“Wakunga wataalamu ni kundi muhimu, wana uwezo wa kutoa huduma bora ya afya ya uzazi inayojumuisha utunzaji wa mama na mtoto katika kipindi chote cha ujauzito na kujifungua.

“Hivyo basi ni muhimu kuwa na mfumo na sera ya uuguzi inayoweka mazingira ya kazi yenye kuridhisha ili kuhakikisha wakunga waliopata mafunzo wanapangiwa na kubakia sehemu za kazi iliyo sahihi,” amesema.

Amesema vifo vya kina mama vimeripotiwa kupungua kwa asilimia 44 ulimwenguni tangu mikakati ya kupunguza vifo ilipoanza miaka 25 iliyopita (1990 –  2015).

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wakunga mwaka huu, yanayotarajiwa kufanyika Uwanja wa Ndege, mkoani Morogoro, anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles