25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa ukoma mbioni kutokomezwa nchini

Na  MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UTAFITI uliofanyika nchini kuhusu ugonjwa wa ukoma umeeleza kuwa kuna matumaini mapya ya kutokuwa na kizazi kisichokuwa na ugonjwa huo kwa kuutokomeza kabisa.

Utafiti huo uliohusisha watu wengi na ulioanzishwa na taasisi ya afya ya kimataifa ya Novartis kwa kushirikiana  na mipango ya kudhibiti ukoma Tanzania na nchi nyingine sita, umechapishwa katika  jarida la Lancet Global Health.

Katika utafiti huu, Tanzania ni nchi pekee kutoka barani Afrika ambayo watu wake walishiriki huku nchi zingine ni Brazil, India, Indonesia, Myanmar, Nepal na  Sri Lanka.

Ofisa wa Kitaifa wa Programu ya Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) kutoka Tanzania ambaye alishiriki  kuandika utafiti huo ni Dk Deusdedit Kamara ambapo alisema Programu ya Leprosy Post-Exposure Prophylaxis (LPEP) ilifuatilia watu 170,000 ambao walikuwa karibu na wagonjwa waliogunduliwa kuwa na ukoma, na kuwatibu 150,000 kati yao na dozi moja ya dawa ya kupambana na TB inayojulikana kama rifampicin, ili kuzuia magonjwa.

Matokeo  ya utafiti huo yanaonyesha kuwa, watu ambao wamekuwa karibu au kishikana kwa namna yoyote na wagonjwa wa ukoma, wakitafutwa na kupewa dozi moja ya dawa ya lkrifampicin,  hii inaweza kwa kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ya bakteria ambao husababisha ukoma.

Matumizi ya dawa hiyo, wanayopatiwa wale ambao wamekuwa karibu na wagonjwa wa ukoma, yanaweza kuzuia kusambaa kwa bakteria wanaosababisha ukoma, ikimaanisha kwamba ikiwa njia hii itapanuliwa ulimwenguni inaweza kutokomeza ukoma katika vizazi na vizazi kwenye nchi ambazo zimefanyiwa utafiti.

Utafiti  huo ulihusisha watu 150,000 kutoka nchi saba, ikiwemo Tanzania unaelezea njia ambayo inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya ukoma ulimwenguni na hivyo kutoa matumaini ya kuutokomeza.

Dk. Ann Aerts, Mkuu wa Shirika la Novartis alisema matokeo haya yanamaanisha kwamba tunaweza kufikia ulimwengu usiokuwa na ukoma.  

 â€œMashirika yasiyo ya kiserikali na wachunguzi ambao walifanya kazi na sisi ili kufanikisha mpango huu wa kihistoria, utawezesha kinga  dhidi ya ukoma baada ya ufafanuzi kutafsiriwa katika sera ya afya ya ulimwengu,” alieleza.

Alisema matumizi ya dawa ya kuzuia ugonjwa wa ukoma yameonyeshwa kupunguza hatari ya kuambukiza ukoma kwa asilimia  60 kwa watu ambao walikuwa karibu au kushikana wagonjwa wa ukoma.

Hata hivyo Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilipendekeza kuingizwa kwa matibabu haya katika Miongozo yao ya 2018 ya Utambuzi, Tiba na Kuzuia Ukoma.

Prof Jan  Richardus, kutokana Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Rotterdam, alisema kuwa utafiti huu umeonyesha kuwa njia hii ya kupunguza maambukizi ni salama, na inawezekana kupitia mipango ya kitaifa ya ukoma. 

“Utafiti wetu unaonyesha kuwa matibabu ya kutafuta watu waliokuwa karibu na wagonjwa wenye ukoma na kuwapatia dawa ili kuzuia maambukizi inakubaliwa vizuri na wagonjwa pamoja na wahudumu wa afya.

“Hatua inayofuata ni kuhakikisha kuwa tiba ya kuzuia maradhi imewekwa katika mipangilio yote ambapo ufuatiliaji wa watu hao waliokuwa karibu wa wagonjwa na uchunguzi umeanzishwa.

Ukoma ni ugonjwa wa kuambukiza wa kudumu unaosababishwa na bakteria aitwaye Mycobacterium leprae.

Ripoti mbalimbali za historia zinaonyesha kuwa ukoma ni ugonjwa ambao umeathiri binadamu tangu miaka mingi iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles