26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa kifua kikuu waua watano

Mwandishi Wetu- Songea

WAGONJWA watano sawa na asilimia 2.4, kati  watu 203 waliobainika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu walioibuliwa  kupitia kampeni ya uelimishaji na uibuaji ya ugonjwa huo inayofanywa na Hospitali ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, wamepoteza maisha kati ya  Julai hadi Septemba, mwaka huu.

Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Wilaya ya Tunduru, Dk. Mkasange Kihongole alisema hayo jana, wakati wa kampeni ya uelimishaji na upimaji wa ugonjwa huo kwa watu na makundi mbalimbali, ikiwemo mama lishe na waendesha bodaboda.

Alisema idadi  ya vifo, ni ongezeko la mtu mmoja ikilinganisha na  watu wanne walipoteza maisha mwaka jana  kati ya 145 waliokutwa na maradhi hayo.

Alisema kwa upande wa watoto walio chini ya umri wa miaka 15 waliokutwa na ugonjwa huo mwaka 2020, walikuwa 75 sawa na asilimia 36.9 na mwaka jana waliokutwa n 25 sawa na silimia 17.2.

Alisema mwaka jana, wahisiwa(waliofanyiwa uchunguzi)wa ugonjwa watu 1,654 waliokutwa na vimelea vya ugonjwa huo, ni 145 na  hadi kufikia   Septemba, mwaka huu  wahisiwa walikuwa 4,073 kati yao 203 walikutwa na maambukizi.

Baadhi ya wananchi, waliishukuru Serikali kwa mpango wake wa kufanya kampeni ya kuibua wahisiwa wa ugonjwa wa kifua kikuu ambao umesaidia sana kuokoa maisha ya wananchi wengi.

Walisema mpango huo, umewezesha kuibuliwa kwa wananchi wengi wenye  ugonjwa huo majumbani ambao hawakufahamu maradhi yanayowasumbua kwa muda mrefu.

Juma Makumbusya, alisema kampeni itaokoa maisha ya  baadhi ya watu wanaogua  ugonjwa huo kwa muda mrefu hasa katika vijiji vilivyopo mpakani  mwa wilaya ya Tunduru na  nchi jirani ya Msumbiji

Juma Makumbusya mkazi wa Kijiji cha Kitanda, alisema, elimu inayotolewa na kitengo cha kifua kikuu imewezesha wazazi  kutambua dalili kwa watoto wadogo, ikilinganishwa  na miaka ya nyuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles