25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ugonjwa wa figo wasumbua duniani

Clara Matimo – Mwanza

WATU milioni 850 wanaishi na tatizo la figo duniani kote na kati ya hao milioni 2.4 wanafariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa sugu wa figo.

Hapa nchini watu zaidi ya 4,300 wanafariki dunia kwa tatizo la ugonjwa sugu wa figo kila mwaka na zaidi ya watu 1,000 wako katika huduma ya kusafisha damu kutokana na tatizo la ugonjwa huo.

Takwimu hizo zilitolewa jijini hapa hivi karibuni na daktari bingwa wa ugonjwa sugu wa figo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC), Ladius Rudovick, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya siku ya figo duniani hospitalini hapo.

Alisema wagonjwa wengi wanaoathirika na ugonjwa sugu wa figo ni wenye kisukari na shinikizo la juu la damu na kwamba hadi sasa BMC inahudumia zaidi ya wagonjwa 600 kwa mwezi.

“Utafiti uliofanywa na BMC mwaka 2012 ulionyesha asilimia 83.7 ya wagonjwa wote wenye kisukari wanaohudhuria hospitalini hapa wanasumbuliwa na ugonjwa sugu wa figo. Pia kati ya watu 100, watu saba hadi 12 wanaishi na tatizo sugu la ugonjwa wa figo,” alisema Dk. Rudovick.

Mmoja wa wagonjwa wanaosafishwa figo BMC, Abdul  Shaban, mkazi wa Mkoa wa Kagera, aliiomba Serikali kupeleka mashine za kusafisha figo katika hospitali za rufaa za mikoa ili iwe rahisi kwa wagonjwa wa maeneo hayo kupata huduma karibu kwa sababu wakati mwingine huwa wanakwama kuwahi siku ya kliniki kutokana na kukosa nauli.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles