24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UGONJWA WA EBOLA WAUA 17 DRC

KINSHASA, DRC


WIZARA ya Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola na kuua watu 17 katika jimbo la Equateur kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka serikalini, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka ulitarajia kuwasili baadae jana kwenye Kijiji cha Ikoko Impenge kilichoathirika jimboni humo.

Dk. Jean Jacques Muyembe, Kiongozi wa maabara ya utafiti wa ugonjwa wa Ebola na magonjwa mengine ya kuambukiza amesema kuna uwezekano mdogo wa ugonjwa huo kusambaa kwenye maeneo mengine

“Hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo ni ndogo kutokana na kwamba vijiji hivyo vilivyoathirika vipo maeneo yasiyofikika kwa urahisi. Ni takriban kilomita 200 msituni na mji wa Mbadaka mji mkuu wa jimbo la Equateur.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ni kwamba kuna visa 21 vya maambukizi ambapo miongoni mwake watu 17 tayari wamefariki dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles