26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

UGANDA YATANGAZA NEEMA KWA WAHUDUMU WA AFYA

KAMPALA, Uganda


WIZARA ya Afya nchini Uganda, imesema kwamba mishahara ya wafanyakazi wote  wa Sekta ya Afya iitapanda  kuanzia mwaka wa fedha ujao.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na Waziri wa Afya , Jane Ruth Aceng, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa sekta hiyo kupitia  Ilani ya Chama tawala Cha  NRM  kuanzia mwaka 2016-2021.

Kwa mujibu wa kiwango cha marekebisho ya mshahara, mshauri mwandamizi ambaye kwa sasa anapata Sh. 3,447,065 atapata sh 4,500,000, mshauri  wa ngazi ya kati ambaye kwa sasa anapata sh3,059,079 atapata Sh 4,200,000 na  muuguzi ambaye mshahara wake ni  Sh.413,158 kuanzia mwaka huo wa fedha ujao atapata Sh.613,158

Mbali na nyongeza hiyo ya mishahara, kwa mujibu wa waziri huyo, pia  wahudumu hao wa Sekta ya Afya watakuwa wakipewa udhamini kwenda kusoma ambao utakuwa ikigharamiwa na Benki ya Dunia.

“Serikali itakuwa ikitoa udhamini katika ngazi mbalimbali kuanzia shahada, stashahada hadi ngazi ya vyeti,”alisema Acen.

Alisema kuwa pia  maofisa hao watanufaika kwa kupewa nyumba za bure, baada ya 68 zinazojengwa katika Mkoa wa Karamoja chini ya msaada wa Serikali ya Italia kukamilika Desemba mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles