24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uganda yaichapa Comoro 20-0

WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya wasichana ya Uganda, imeichapa Comoro mabao 20-0 katika michuano ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Baraza la Vyama vya kwa nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), yanayoendelea nchini Mauritius.

Katika mchezo huo uliopigwa jana Uwanja wa Anjalay. Mabao ya Uganda yalifungwa na Margret Kunihira aliyefunga matano dakika ya 2, 3, 22, 25, 61, Juliet Nalukenge mabao saba dakika ya 10, 19, 26, 31, 34, 54, 90.

Mengine yalipachikwa na Shakira Nyinagahirwa alifunga matatu dakika ya 31, 38, 44, Gillian Akadinda dakika 45 na Fauzia Najjemba aliyefunga manne dakika ya 45, 77, 79, 84.

Katika mchezo mwingine, Zambia iliwafunga wenyeji Mauritius mabao 8-0 Uwanja wa St. François Xavier.

Kwa matokeo hayo, Zambia na Uganda zimetinga nusu fainali, baada ya kufikisha pointi saba kila mmoja  kupitia michezo mitatu zilizoshuka dimbani, zikishinda mechi mbili mbili na kupoteza moja.

Timu hizo zilizopo kundi A, zinasubiri washindi wa leo kutoka kundi B, Madagascar ikicheza na Afrika Kusini huku Shelisheli ikikabiliana na Botswana.

Katika michuano hiyo inayoshirikisha timu nane, Juliet Nalukenge wa Uganda, ndiye anayeongoza kwa mabao akifunga 14, aliyofunga katika mechi tatu, akifuatiwa na Oyisa Marhasi wa Afrika Kusini aliyecheza michezo miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles