31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uganda: Tume ya mawasiliano yaagiza kufungwa kwa vituo 13 vya redio na televisheni

Tume ya Mawasiliano nchini Uganda imeagiza kufungwa kwa vituo 13 vya radio na televisheni pamoja na kufutwa kazi baadhi ya wanahabari kwa kupotosha na kuchochea ghasia kwa kutangaza taarifa zilizo na ujumbe tofauti.

Tume hiyo inasema kuwa vyombo hivyo vya habari vilikiuka kanuni ya kifungu cha 31 ibara ya 4 ya sheria ya mawasiliano ya Uganda ya mwaka 2013. Japokuwa haikufafanua jinsi sheria hiyo ilivyokiukwa katika agizo lake kwa vyombo hivyo vya habari.

Tume inataka hatua dhidi ya wazalishaji vipindi, wahariri wa kuu na wasimamizi wa matangazo kusimamishwa kazi katika mda wa siku tatu.

“Hii ni kufuatia jinsi zinavyoshughulikia mada zinazorushwa hewani wakati wa matangazo ya moja kwa moja, Habari za hivi punde na Habari zingine kwa ujumla bila kuzingatia kanuni ,” iliongeza Tume ya UCC.

Chama cha wanahabari nchini Uganda (UJA) kimeelezea kughadhabishwa na hatua hiyo na kusema kuwa wanahabari karibu 30 wanakabiliwa na tishio la kufutwa kazi na hilo halitakuwa na athiri kwa taaluma zao tu bali mamilioni ya waganda watakosa huduma ya kupashwa habari.

Kwa upande mwingine, kuna madai kuwa huenda hiyo imetokana na mtangazo ya moja kwa moja ya kukamatwa na kushtakiwa kwa Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Kyagulanyi kwa sasa anazuiliwa rumande na anatarajiwa kufikishwa tena mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Buganda Road leo Alhamisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles