23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Ufaransa kusaidia sudan kulipa madeni

Paris, Ufaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo anatarajia kukutana na viongozi wa Afrika, wanadiplomasia na wafadhili wa kifedha kwenye mkutano wa kilele mjini Paris, unaolenga kuisaidia Sudan baada ya miaka mingi ya machafuko kufuatia utawala wa kimabavu.

Wakuu kadhaa wa nchi za Afrika watajadili mzigo wa madeni unaoikumba Sudan, ili kuisaidia serikali ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdock anayeiongoza nchi hiyo kwenye mpito baada ya dikteta wa muda mrefu Omar al-Bashir kupinduliwa mwaka 2019.

Hapo kesho Jumanne, mkutano wa kilele wa mataifa ya Afrika, utajaribu kujaza pengo lililopo la takriban dola bilioni 300 kutokana na janga la Covid 19.

Washiriki wa mikutano yote miwili watahudhuria wenyewe, hali inayoashiria kurejea kwa mikutano ya watu kujumuika pamoja, tofauti na mikutano kwa njia ya video kufuatia covid-19.

Mikutano hiyo pia ni nafasi kwa Macron kujionesha kama kiongozi ambaye ushawishi wake umetanuka hata kwenye nchi za Afrika zisizozungumza Kifaransa.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria mikutano hiyo ni Paul Kagame wa Rwanda na Abdel FAttah al-Sissi wa Misri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles