24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 21, 2024

Contact us: [email protected]

UDOM wanadi tiba lishe kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimewataka Watanzania kuzingatia umuhimu wa lishe bora ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Chuo hicho kinatumia Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora pamoja na kufanya uchunguzi wa awali wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumza Agosti 3,2024 kwenye maonesho hayo Mkufunzi Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii, Kassim Mohamed Ally, amesema wanatoa elimu ya tiba lishe kwa kutumia chakula ambayo inatoa mwongozo sahihi wa jinsi ya kula.

“Wanafunzi wanasoma kozi hii kwa miaka minne na mwaka mmoja wanakwenda kwenye mazoezi ya vitendo hospitali au sehemu watakayochagua, tunawafundisha jinsi lishe inavyofanya kazi kwa kuunganisha na sayansi, muundo wa mwili na ufanyaji kazi wa mwili.

“Wanajifunza kutambua chakula unachokula ndani yake kuna nini, kinaenda kuchakatwa vipi na sehemu gani inachakatwa, tunaichukua sayansi na kuileta kwenye uhalisia,” amesema Ally.

Amesema pia wanafanya uchunguzi wa vipimo vya awali kama vile uwiano wa urefu na uzito, sukari, presha na vingine na kutoa ushauri juu ya lishe bora.

Kwa mujibu wa Mkufunzi huyo, kesi nyingi wanazozipata kwa watu mbalimbali wanaofanyiwa vipimo vya awali ni uzito kuongezeka na kwamba wamekuwa wakiwashauri jinsi ya kuupunguza kwa kuzingatia makundi muhimu ya vyakula.

“Wataalam wa lishe wanaoibuka ni wengi lakini ni muhimu tuangalie tunayoshauriwa kwa sababu tunakutana na watu wanasema wameshauriwa wasile vyakula fulani lakini baadaye wanajikuta wanapata athari kama za vidonda vya tumbo.

“Wanawake wanaharibu mfumo mzima wa homoni, hedhi zao zinakuwa haziko vizuri kwahiyo, Watanzania wawafuate wataalam wa tiba lishe ambao wana vigezo,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles