25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Udhamini unavyohatarisha ushindani wa timu za kikapu Taifa Cup

Na WAANDISHI WETU



MAWAZO ya wadau wengi wa mchezo wa kikapu hivi sasa, makocha na walimu wa timu mbalimbali za mchezo wa kikapu mikoa tofauti ni michuano ya Taifa Cup, ambayo mwaka huu itaanza kutimua vumbi Desemba Mosi huko Simiyu.

Jumla ya timu 25 za wanawaume na wanawake kutoka mikoa toafuti hapa nchini zinatarajiwa kushuhudiwa zikichuana kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Katika michuano hiyo itakayosimamiwa na kuendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), kila timu itashiriki ikiwa na idadi ya wachezaji 15.

SPOTIKIKI linakuletea maandalizi ya mikoa yenye ushindani wa hali ya juu kwenye mchezo wa kikapu hapa nchini, kuelekea kwenye michuano hiyo ya kitaifa.

DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa TBF, Michael Mwita, anasema kuwa maandalizi yamefikia katika hatua nzuri, kwani tayari timu zinaendelea na mazoezi.

Anasema kikubwa kinachowasumbua kwa sasa ni wadhamini, ambao watazisapoti timu hizo kwenye maandalizi kuelekea kwenye michezo hiyo.

“Wale wadau ambao wameonyesha nia ya kusapoti timu zetu huu ndio muda wao muafaka wa kuyatekeleza yale, ambayo wameahidi, tunaomba na wengine wenye malengo ya kuinua mchezo huu hapa nchini wajitokeze.

Udhamini

Mwita anasema bajeti yote ya michuano hiyo ni milioni 50, lakini serikali ya Simiyu imepunguza, baadhi ya garama ikiwamo chakula na malazi,  hivyo wao kama shirikisho wanatakiwa kusaka milioni 20.

“Tuna tafuta milioni 20 kwani serikali ya Simiyu imeshapunguza matumizi, tunawaomba wale wadau ambao wamehidi katika hili watoe sasa kwa muda umeshafika na siku zilizobaki ni chache.

Wenyeji Simiyu

Anasema kwa upande wa Mkoa wa huo  maandalizi ya kuweka sawa mazingira bora ya kuweza kuwalaza wachezaji, yanaendelea vema.

Anasema pia hali ya hewa niyakawaida na wachezaji wote wanaweza kuimudu, hivyo wasipate hofu bali wajiandae kwa ushindani ili kutoa burudani ya kutosha mkoani Simiyu.

“Hali ya heya ya kawaida na ninaamini wataifurahia, maandalizi yanaendelea vizuri na ukiangali serikali ndio imechukua sehemu kubwa ya udhamini, hivyo hatuna shaka na Mkuu wa Mkoa Antony Mtaka, kwani hakuna kitakachoharibika,”anasema Mwita.

TANGA

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mkoani Tanga (TRBA), Khamisi Jafari anasema timu za mkoa huo kwa

upande wa wanawake na wanaume, zimeanza maandalizi zikiwa na lengo la kuibuka na ushindi.

“Labda niseme kwamba msimu huu malengo yetu makubwa ni kuchukua ubingwa, lakini pia kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mashindano hayo hata tuweze kumaliza tukiwa nafasi za juu kwa timu zote wavulana na wasichana.

 

Udhamini

Anasema licha ya kuanza maandalizi, lakini hivi sasa wanakabiliwa na  upatikanaji wa fedha, ambazo

zitawawezesha kushiriki mashindano hayo bila kuwepo vikwazo vya namna yoyote.

“Tumejitahidi kupeleka barua kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga, kuona iwapo tunaweza kupata msaada ambao ndio utakuwa chachu kubwa kwetu kwani tunauhitaji mkubwa sana.

 

Wasimamizi

Anasema wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia kanuni na sheria katika michuano hiyo, kwani kitendo cha timu kutumia wachezaji kutoka mikoa mengine inawavunja moyo na kuwanyima wahusika nafasi ya kuonyesha viwango.

MWANZA

Kuelekea michuano ya Taifa Cup, tayari mkoa wa Mwanza umetangaza kikosi cha awali cha wachezaji 31 wa timu ya wanaume.

Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza(MRBA), Haidari Abdul anasema tayari kikosi kutoka mkoani humo kimeanza maandalizi wiki iliyopita kwenye Viwanja vya kisasa vya Mirongo, chini ya makocha, Paschal Nkuba na Kizito Bahati.

“Hadi sasa wachezaji waliochaguliwa wanafika 30, lakini watachunjwa na kupatikana 15 watakaounda kikosi kizima, tunaamini  nyota watakaochaguliwa watafanya vizuri kutokana na uwezo walio nao, kwasababu viongozi wamezingatia zaidi kipaji cha kila mchezaji.

Udhamini

Anasema kuwa licha ya kuwa hivi sasa wanaelekea kwenye mashindano ya taifa, bado wadu wamekuwa wazito kuonyesha ushirikiano wa karibu kwa timu.

Anasema hamasa iliyokuwepo awali imepungua, mchezo huo umekosa wadhamini na kupelekea wakati mwingine ligi ya mchezo huo ngazi ya mkoa kutochezeka na timu zake za mkoa kushindwa kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa kutokana na ukata.

Makala hii imeandikwa na Glory Mlay, Oscar Assenga, Damian Masyenene

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles