25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Uchunguzi sumu mwilini mwa Mangula waendelea

CHRISTINA GAULUHANGA na TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema  uchunguzi  wa tuhuma za kuwekewa sumu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula bado haujakamilika.

Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa waandishi alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo bado linafanyiwa uchunguzi ili kuwea kubaini undani wake.

“Bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio la kulishwa sumu kwa Mangula na msitarajie kuwa kuna siku tutaeleza uchunguzi huo mbele yenu,” alisema Mambosasa.

Awali ilidaiwa kuwa Februari 28, mwaka huu, Mangula alidondoka ghafla katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali ambapo ilitoa adhabu kwa wanachama watatu waliokuwa na tuhuma za ukiukwaji wa maadili ndani ya chama hicho.

Katika kikao hicho, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kanuni ya maadili na uongozi.

Machi 9, mwaka huu alipozungumza na waandishi, Mambosasa, alisema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, walibaini ndani ya mwili wa Mangula kulipatikana sumu.

Alisema kuwa jeshi hilo litachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kupanga, kuratibu au kusimamia utekelezaji wa uhalifu huo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles