24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Uchumi wa Tanzania waongezeka kufikia asilimia 5.2 Robo ya Tatu ya Mwaka 2021

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema katika kipindi cha Robo ya Tatu ya mwaka 2021 Julai hadi Septemba, Uchumi wa Tanzania umeongezeka hadi kufikia kiwango cha asilimia 5.2 kutoka asilimia 4.4 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Aidha, pato la taifa  kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi sh trilioni 37.0 kutoka Sh Trilioni 34.5 kipindi kama hicho mwaka 2020 ambapo pato halisi la Taifa  liliongezeka hadi Sh trilioni32.0 mwaka 2021 kutoka Sh trilioni 30.3 katika kipindi kama hicho 2020.

Hayo yameelezwa leo Januari 4,2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Daniel Masolwa, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  ukuaji wa uchumi kipindi cha Julai hadi Septemba 2021.

Masolwa amesema katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2021 Julai hadi Septemba, uchumi umeongezeka hadi kufikia kiwango cha asilimia5.2 kutoka asilimia 4.4 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Aidha, pato la taifa kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi Sh trilioni 37.0 kutoka Sh trilioni34.5 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Vilevile, pato halisi la Taifa  liliongezeka hadi Sh trilioni32.0 mwaka 2021 kutoka Sh trilioni30.3 katika kipindi kama hicho 2020.

“Katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2021 pamoja na changamoto za UVIKO- 19 uchumi umeendelea kuimarika ambapo shughuli za huduma ya malazi na chakula iliongoza kwa kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 14.3,”amesema Masolwa.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ukuaji huo ulichangiwa na kuongezeka kwa watalii 243,565 walioingia nchini kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2021 ikilinganishwa na watalii 72,147 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Hata hivyo, makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2021 kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF) mwezi Oktoba 2021, uchumi wa Dunia kwa mwaka 2021 ulitarajiwa kukua kwa kiwango cha asilimia 5.9 huku kwa mwaka 2022 ukieendelea kubaki katika kiwango cha asilimia 4.9 zilizokuwazimekadiriwa awali.

Amesema ukuaji wa uchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kipindi cha Julai- Septemba 2021 umeendelea kuimarika kutoka kiwango hasi cha ukuaji hadi kiwango chanja.

Amesema kwa upande wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uchumi umekadiriwa kukua hadi asilimia 3.7 katika kipindi cha Julai- Septemba 2021

Kwa upande wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, Masolwa amesema makadirio ya ukuaji wa uchumi katika nchi hizo yalionesha Oktoba 2021 kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi hadi asilimia 3.7 kwa mwaka 2021.

“Makadirio haya yanatarajia kuongezeka  kutokana na kuimarika  kwa usafirishaji wa bidhaa nje ambazo zimesaidia kukabiriana na madhara kuagiza zaidi bidhaa za chanjo ya UVIKO-19 kutoka nje,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles