UCHANGIAJI DAMU BADO TATIZO NCHINI

0
1062

Na VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM


UCHANGIAJI wa damu katika benki ya taifa ya mpango wa damu salama ni muhimu  kunusuru maisha ya Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini, imeelezwa.

Hivyo Watanzania wameaswa kuendelea kujitolea katika utoaji na uchangiaji wa damu kwa kuwa mahitaji ya damu bado ni makubwa.

“Jukumu la kuchangia damu limapaswa kuwa na kila mtanzania, kila kampuni, kila taasisi, kila sekta na  kila mmoja wetu,”  alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mrisho Yassin,

Alikuwa akiongoza wafanyakazi wa Kampuni ya Swisspor walipokuwa wakichangia damu kwa waratibu wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama jana.

Alisema   huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa kampuni yao kuchangia damu katika kuokoa maisha ya Watanzania.

“Tumejitahidi kuhamasisha wafanyakazi wetu   ofisini kuendelea kujitolea damu kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa wananchi tunaowatumikia kwa uaminifu mkubwa.

“Mahitaji ya damu nchini bado ni changamoto kubwa, tunapaswa kuweka nguvu   kuwaelimisha wananchi kuendelea kuchangia damu  kunusuru majeruhi wa ajali na wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji kwa kuboresha benki ya damu ya taifa.”alisema Yassin.

Mmoja wa wafanyakazi wa Swissport, Gilead Marisa  alisema   yeye ana tabia ya kutoa damu   kusaidia wanawake wanaokwenda kujifungua   na majeruhi wa ajali   na watu mbalimbali wenye shida ya damu salama.

Aliitaka  jamii kujenga mazoea ya kuchangia damu kuokoa maisha ya watu wengi.

Ofisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Fatuma Mjungu alisema   kwa  mwaka, mahitaji ya damu nchini ni  chupa 300,000.

Alisema  kila mkoa umejiwekea lengo la kuchangia chupa 100 za damu salama ambako kwa mikoa yote 25 ya Tanzania bara zitapatikana chupa 2,500.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here