25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UBELGIJI HIYOOO KOMBE LA DUNIA URUSI

PIRAEUS, Ugiriki

TIMU ya taifa ya Ubelgiji imekuwa taifa la kwanza kutoka Ulaya kujiunga na wenyeji Urusi, katika kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia.

Hatua hiyo imekuja baada ya juzi timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Ugiriki wa mabao 2-1, kupitia kwa Jan Vertonghen na Romelu Lukaku.

Mabao yote matatu yalifungwa katika dakika ya tano kipindi cha pili, Vertonghen akitangulia kwa kuiweka Ubelgiji kifua mbele.

José Carlos Gonçalves Rodrigues wa Ugiriki, almaarufu kama Zeca, aliipatia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 73, lakini dakika ya 74 Lukaku akaifungia Ubelgiji bao la ushindi kwa kichwa.

Ushindi huo uliifanya Ubelgiji kuongoza katika kundi H na alama 8, wakiwa bado na michezo miwili ya kucheza.

Ubelgiji wamejiunga na Brazil, Iran na Japan katika kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia, huku Urusi wakijipatia nafasi ya moja kwa moja kwa kuwa ni wenyeji wa michuano hiyo.

Timu ya Bosnia-Herzegovina imeipita Ugiriki na kujipatia nafasi katika michezo ya kufuzu kwa njia ya mtoano.

Mafanikio ya timu hiyo yalitokana na Edin Dzeko kufunga mabao mawili yaliyowapatia ushindi wa mabao 4-0 na kujinyakulia nafasi ya pili katika kundi hilo nyuma ya Ubelgiji.

Mabao mengine ya vijana hao wanaonolewa na kocha, Mehamed Bazdarevic, yalifungwa na Kenan Kodro na Senad Lulic na kufikisha alama 14, na kuwa na alama moja zaidi ya Ugiriki.

Uswizi ilisalia na alama tatu mbele ya mabingwa wa Ulaya, Ureno, baada ya wote kupata ushindi siku ya Jumapili.

Bao la kujifunga kipa wa Uswizi, Andris Vanins, pamoja na lile la mshambuliaji Blerim Dzemaili, ambaye hapo awali alikosa penalti kabla ya bao la penalti la Ricardo Rodrigue, yaliipatia timu hiyo ya Uswizi ushindi mnono huko Latvia.

Timu ya Ureno ilipata ushindi baada ya Tamas Priskin kutolewa uwanjani na kupata ushindi wa bao 1-0 kupitia Andre Silva dhidi ya Hungary.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles