28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Ubalozi wa Marekani wamlilia Mengi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetuma salamu za rambirambi na pole kwa familia kutokana kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Media na mfanyabiashara Dk. Reginald Mengi.

Dk. Mengi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Alhamisi Mei 2, nchini Dubai alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika taarifa iliyotolewa leo na ubalozi huo imeeleza namna walivyopokea kwa majonzi taarifa za kifo cha Dk. Mengi.

“Tulipata fursa ya kufanya kazi na Dk. Mengi katika siku zilizopita na kwa hakika mchango wake katika ukuaji wa muda mrefu wa uchumi na maendeleo ya Tanzania ni mkubwa na muhimu.

“Tunatoa pole na rambirambi zetu za dhati kwa familia na rafiki zake na kuungana na watu wa Tanzania katika kuomboleza msiba huu mzito,” imesema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles