25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ubalozi wa China waomboleza waliopoteza maisha kwa corona

Dar es salaam

Ubalozi wa China nchini leo, umeungana na wenzao kwenye taifa la kwanza kukumbwa na virusi vya corona, kuomboleza waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo wa homa kali ya mapafu.

Maombolezo hayo yameongozwa na Balozi wa China nchini, Wang Ke, yaliyofanyika kwa kupandisha bendera nusu mlingoti.

Katika maombolezo hayo, Balozi Ke, Katibu Mkuu wa Jumuhiya ya Kuendeleza Urafiki kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wawakilishi wengine kutoka Ubalozi wa China na makampuni nchini Tanzania, wametoa heshima kwenye makaburi ya wataalamu ya kichina nje ya Dar ya Salaam, waliofariki dunia wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).Tanzania.

Mapema leo China imefanya maombolezo ya nchi nzima kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona. 

Bendera za taifa hilo zimepepea nusu mlingoti nchi nzima pamoja na kusitisha shughuli zote za burudani. 

Siku hiyo ya maombolezo imeambatana na kuanza kwa sherehe za kila mwaka za kuwakumbuka mababu wa zamani nchini China. 

Sherehe hizo zimeanza kwa nchi kukaa kimya kwa muda wa dakika tatu, ili kuomboleza waliofariki, wakiwemo wafanyakazi wa afya waliokuwa mstari wa mbele na madaktari. 

Magari, treni na meli zilipiga honi na sauti za ving’ora zilisikika hewani. 

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wametoa heshima zao za kimya mbele ya bendera ya taifa mjini Beijing. 

Zaidi ya watu 3,000 China bara walifariki dunia kutokana na COVID-19.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles