Ubakaji watoto wazidi kuongezeka

0
881
Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba.

Na MANENO SELANYIKA, DAR ES SALAAM

MATUKIO ya watoto kubakwa na kulawitiwa yamezidi kuongezeka kwa kasi hadi kufikia watoto 2,571 mwaka huu kutoka 1,585 mwaka jana.

Takwimu zilizotolewa juzi katika maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha -Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa kuanzia Januari ilikuwa watoto 180 hadi kufikia Machi mwaka huu watoto 1,765 walifanyiwa vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba alisema idadi ya watoto wa kiume kulawitiwa inaongezeka kwa kasi ya ajabu.

“Matukio ya watoto wa kiume kulawitiwa yameendelea kuonezeka kwa kasi ya ajabu huku wahusika na ukatili huo wakirandaranda bila kuchukuliwa hatua za msingi kwa hoja ya uhusiano wa karibu kati ya mtoto na aliyemlawiti,”alisema Bisimba.

“Ripoti inaonyesha kuwa asilimia 49 ya vitendo hivyo hufanyika nyumbani,asilimia 23 hufanyika njiani wakati wa kwenda au kurudi shuleni na asilimia 15 hufanyika shuleni,”alisema

Katika maadhimisho hayo LHRC walitoa msaada wa mahitaji ya watoto wanaoishi katika kituo hicho.

Akishukuru msaada huo, Ofisa Mfawidhi wa watoto katika kituo hicho, Betres Laurence alisema kuwa serikali, jamii ma wadau kwa pamoja wanawajibu wa kushirikiana ili kutatua changamoto za watoto.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alisema kati ya hao, watoto wa kike sawa na asilimia 43 walikuwa wamebakwa  na 24 wa kiume sawa na asilimia 7.9 walikuwa wamelawitiwa.

“Kwa sasa Mazingira  mengi yanayowazunguka watoto hayapo  salama  kutokana na  watoto  kushindwa  kuhimili  changamoto hiyo wazi  wachukue tahadhari dhidi ya  Mazingira  wanayokuwepo watoto baada ya muda wa masomo..

“Vitendo hivyo  huanzia majumbani  na ndiko  kunakoongoza  kwasababu kwa wakati huo  walimu hawapo  katika nafasi  ya kujua  nini  wafanyacho  watoto nje ya shule,’’alisema Tabu.

Aidha aliwataka wazazi  na walezi kuchukua tahadhari dhidi ya mazingira  yanayowazunguka  watoto hususan   kuchangamana na watu walio wazidi umri.

“Wazazi  na walezi  mjenge mazingira ya  ukaribu,upendo huduma ya  msaada wa kisaikolojia  unaogusa na kujenga  mawazo  yao katika mihemko  na tabia za watoto  ikiwa ni pamoja na masuala ya  kijamii yanayogusa elimu, mazingira, mila,desturi pamoja na mahusiano yao na wenzao”alisema.

Kulingana na sheria ya mwaka 2009 ni jukumu la kila mmoja kutoa taarifa za ukiukwaji wa haki za mtoto, ukatili  na udhalilishaji ili hatua za kisheria ili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here