25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ubabe wa China wailazimu Japan kurusha ndege zake

japanTOKYO, JAPAN

SERIKALI ya Japan imesema ililazimika kurusha ndege zake angani juzi baada ya ndege nane za China kuruka kati ya visiwa vya vyake.

Ndege hizo zinaozodaiwa kuwa zile za kurusha mabomu, kufanya uchunguzi pamoja na kivita ziliruka juu ya visiwa hivyo vya Miyako, Okinawa na Miyakojima.

China imesema ndege 40 zilihusika katika kile inachokitaja kuwa zoezi la kawaida.

Ndege hizo hazikupita katika anga ya Japan, lakini hatua hiyo inaonekana kuwa maonyesho ya ubabe wa China.

Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Japan kusema itashiriki katika zoezi la pamoja na wanamaji wa Marekani katika Bahari ya kusini mwa China.

Msemaji mkuu wa Japan amesema taifa hilo linachunguza hatua hizo za China kwa karibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles