23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Uamuzi wa JPM uibue na mengine

Andrew Msechu

PRESHA imeshushwa! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Rais Dk. John Magufuli kutoa uamuzi wa kurejesha kikokotoo cha zamani cha malipo ya wastaafu, baada ya malalamiko na manung’uniko waliyokuwa nayo wafanyakazi nchini.

Rais ametangaza uamuzi huo juzi katika kikao chake na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, mifuko ya hifadhi ya jamii na waajiri.

Uamuzi huo ameondoa kanuni mpya za malipo hayo ambazo zilitokana na sheria mpya iliyopitishwa na Bunge ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwa miwili ambayo ni PSSSF na NSSF.

Bunge ndiyo chanzo cha kuundwa kwa kanuni mpya za kikokotoo cha mafao ya wastaafu, ambazo zilitoa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 50 hadi 25 na mengine kuelekezwa kwenye nyongeza ya malipo ya kila mwezi.

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka ndiye aliyesimamia mabadiliko hayo, na katika uandaaji, upitishaji na kuanza kutekelezwa kwa kanuni mpya za kikokotoo cha malipo ya wastaafu, hakuwa peke yake.

Kanuni hizo zilipata baraka za wizara husika, kwa maana hiyo zilipata baraka za Serikali na kwa kuwa nia ilikuwa moja, zikaanza kutumika kwa wastaafu nchini.

Katika usimamizi wa kanuni hizo, malalamiko kutoka pande mbili, wawakikishi kutoka vyama vya wafanyakazi na wanasiasa kutoka upande wa upinzani ndio walioonesha kula pamoja, kulia pamoja katika kupinga kanuni hizo kandamizi.

Licha ya malalamiko hayo, si waziri husika, kiongozi mkuu wa SSRA wala mwanachama yeyote wa CCM aliyejitokeza hadharani kuonesha kwamba kuna tatizo katika kanuni na utaratibu huo mpya wa ukokotoaji wa mafao.

Tulichoshuhudia kila kona, ilikuwa ni kauli na nyimbo za kusifia utaratibu huo na kusifia Serikali katika kuhakikisha inasimamia kikamilifu kanuni hizo, ambazo kimsingi zilikuwa ni dhuluma iliyolalamikiwa na wafanyakazi.

Ni Rais Dk. Magufuli pekee aliyeamua kukutana na viongozi hao na kutoa uamuzi uliohitimisha malalamiko hayo kwa kuweka kipindi cha uangalizi cha miaka mitano, ili kupata suluhu ya maeneo yenye matatizo.

Katika mtiririko mzima wa matukio hayo, ni wazi kwamba aliyetakiwa kuwajibika au kuwajibishwa si Mkurugenzi wa SSRA pekee, bali wapo waliotakiwa kuambatana naye katika jambo hilo.

Ni wazi kwamba kuwajibishwa kwa Isaka kuna ishara ya kuwa sadaka kwa kupisha uundwaji wa kanuni mpya kwa kikokotoo kipya, basi na iwe sadaka iliyo njema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles