TYSON AMPA UBINGWA FLOYD MAYWEATHER

0
554

NEW YORK, MAREKANIBINGWA wa zamani wa ngumi uzito wa juu duniani, Mike Tyson, ameweka wazi kuwa Floyd Mayweather ana nafasi kubwa ya kuwa bingwa kwenye pambano la Agosti 26, mwaka huu dhidi ya mpinzani wake Conor McGregor.

Pambano hilo la kihistoria linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Angeles na tayari bei ya tiketi imewekwa wazi, huku kiingilio cha chini kabisa kikiwa ni dola 500 sawa na milioni 1,096,300.

Kiingilio cha juu kikitajwa kuwa ni dola 10,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 21 za Kitanzania. Mabondia hao wameanza kutambiana kuelekea pambano hilo huku McGregor akidai kuwa atahakikisha anamaliza mchezo huo katika raundi ya nne.

Tyson alifanya mazungumzo kwenye kipindi cha runinga cha Pardon My Take, alisema kwamba, McGregor hana nafasi yoyote ya kushinda katika pambao hilo kwa kuwa uwezo wake ni mdogo.

“Kuna uwezekano mkubwa McGregor akapoteza maisha kwenye pambano hilo. Sijui watatumia sheria gani, lakini imani kubwa ni kwamba, Mayweather atashinda kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa.

“McConor ana uwezo mkubwa, lakini nafasi ya kushinda ni ndogo. Endapo Mayweather atatumia nafasi vizuri kwenye mchezo huo, basi anaweza kushinda kwa KO,” alisema Tyson.

Tyson amesisitiza kwamba pambano hilo litakuwa la aina yake kutokana na ushindani wa wawili hao na inawezekana likawa tofauti na lile la Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao, Mei 2015.

“Wengi wanatarajia kuona makubwa kwenye pambano hilo, hawatarajii kama yale ambayo yalitokea kwenye pambano la Maywether dhidi ya Pacquiao ambapo mshindi alipatikana kwa pointi, Agosti lazima mtu aonekane akipigwa na si ushindi wa pointi,” aliongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here