Tyrese ashindwa kesi ya mtoto wake

0
1269

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa muziki na filamu nchini Marekani, Tyrese Gibson, ameshindwa kesi ya kumtaka mtoto wake wa kike Shayla asicheze mpira.

Mkali huyo wa muziki wa RnB, alifikishana mahakamani na mama wa mtoto wake, Norma Gibson ambaye alimruhusu mtoto wake kucheza mpira, lakini Tyrese alisema hayupo tayari kumwona mtoto wake huyo akicheza mpira.

Kwa mujibu wa Mahakama mjini Los Angeles, Norma Gibson, ameshinda, hivyo mtoto wao huyo mwenye umri wa miaka 11 anaruhusiwa kucheza mpira.

Tyrese mwenye umri wa miaka 38, alikuwa anamtaka mtoto wake kujikita katika mambo ya msingi akiwa shuleni na si kucheza mpira, lakini mama wa mtoto huyo alikuwa anasapoti mwanawe kucheza mchezo aupendao na tayari amefanikiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here