27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

“Twenzetu na Dorice Mgetta Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa”

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

Jumapili ya Novemba 27, mwaka huu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)utafanya Uchaguzi wake Mkuu wa kuwapata viongozi mbalimbali ikiwamo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea Novemba 15, mwaka huu na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kenani Kihongosi (MNEC), Wagombea katika nafasi ya mwenyekiti ni wanne ambao ni Farid Mohamed Haji, Kassim Haji Kassu, Mohammed Ali Mohammed(Kawaida) na Abdallah Ibrahim Natepa.

Dorice Mgetta.

Upande wa wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Khadija Khalid Ismail, Dorice John Mgetta, Victoria Charles Mwanziva na Rehema Sombi Omary.

Tukiitazama nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM ni bayana kwamba kulingana na kasi na mabadiliko ya sasa ya mfumo wa siasa sambamba na uchapa kazi unaotekelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, hakuna shaka kwamba Dorice Mgetta ni mtu sahihi katika kuchangiza kasi hiyo.

Kwani ni wazi kuwa ustawi wa chama cha Mapinduzi unategemea sana jitihada za hali na mali za wanachama wake, na hilo ni moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakitekelezwa na Dorice katika kuhakikisha kuwa chama kinaimarika kiuchumi, kisiasa na kiraslimali.

Hivyo, hiyo ni moja kati ya sifa nyingi zinazompa uhalali wa kutaka kuvaa viatu vya makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa nafasi ambayo anaonyesha kuimudu vilivyo iwapo atachaguliwa na wanachama Novemba 27, 2022.

Dorice ni nani?

Dorice Mgetta ni msichana wa Kitanzania(28) aliyebobea katika taaluma ya Sheria na Mwanadiplomasia wa Uchumi.

Hata hivyo, mbali na kofia hizo, Dorice ni Mjasiriamali na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Serve Tanzania Foundation iliyojikita kusaidia na kuwahamasisha Wanawake na Vijana katika nyanja ya kilimo na ujasiriamali nchini.

Kama hiyo haitoshi, Dorice ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Siasa

Dorice ni Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwa kuzaliwa na ni Mwanajumuiya ya Umoja wa UVCCM ambaye kwa karibu amekuwa akishiriki shughuli zote za ujenzi wa chama na raslimali.

Pia amekuwa akihakikisha kuwa katika kipindi chote cha maisha yake ya ndani ya Jumuiya na CCM ana kipambania chama kukamilisha dhamira yake kuu ya kushidna chaguzi na kuunda Dola.

“Ustawi wa Chama Cha Mapinduzi unategemea sana jitihada za hali na mali za wananchama wake, mimi kama mwanachama nimekuwa nikijitahidi kutekeleza wajibu huo wa kuhakikisha chama chetu kinaimarika kiuchumi, kisiasa na kiraslimali.

“Pia nimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za chama ikiwamo uchangiaji wa ujenzi wa nyumba ya Katibu Mkuu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo na Kinondoni mkoani Dar es Salaam. Sambamba na hayo nimeshiriki ujenzi wa tawi la CCM Kunduchi.

“Aidha, nimeratibu mafunzo ya uongozi kwa wenyeviti wa wilaya zote nchini yaliyofanyika Ihemi mkoani Iringa,” anasema Dorice.

Dorice anaongeza kuwa amejitolea kwa karibu kufanya kazi za Chama chini ya idara ya SUKI, kazi ambayo yeye mwenyewe anasema kimsingi zimemjenga na kumuimarisha vyema kiuongozi kupitia idara hiyo (SUKI).

“Tumefanikiwa kufanya kazi ya uratibu wa Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Nyerere, Kibaha Pwani. Pamoja na kuunda mtaala wa masomo wa chuo hicho,” anasema Dorice.

Balozi wa katika jamii

Ikumbukwe kwamba pamoja na kujihusisha na siasa bado Dorice anabaki kuwa mwanajamii.

Hiyo ndiyo imekuwa na msukumo kwake yeye katika kujihusisha na shughuli za kijamii.
“Mwanajamiii na Mwana CCM anapaswa kuwa mtu wa karibu na jamiii anayoishi. Kwa kuzingatia hilo nimekuwa nikishiriki kufanya shughuli ndani ya jamii.

“Miongoni mwa kazi hizo ni kufanya uhamaisishaji wa kimtandao (Women at Web), kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za kitehama na hawadhalilishwi kwenye mitandao ya kijamiii, vivyo hivyo ni muanzilishi na Mjumbe wa jukwaa la kimtandao wa mabinti wanaofanya biashara na ujasiriamali la Young Women Enterprineur(YWE).

“Pia nimekuwa Mjumbe na mdau wa mradi wa BBT (BEALDING A BETTER TOMMOROW) chini ya Wizara ya Kilimo huku pia nikiwa mshiriki wa kuhamasisha vijana na wanawake kuhesabiwa sensa ya watu na makazi iliyofanyika Oktoba 23, mwaka huu,” anasema Mwanamageuzi hiyo wa Chama Cha Mapinduzi.

Tunapoongelea suala la uongozi bora na maendeleo kwa vijana, hatuwezi kumuacha Dorice Mgetta.

Kwani anajiamini, ana juhudi na mchapa kazi na amekuwa akiwakilisha vema wanawake na vijana katika bodi ya TanTrade.

Ukatili wa kijinsia

Dorice Mgetta pia amekua mstari wa mbele katika kupinga ukatili wa kijinsia katika mitandao ya kijamii na kuhamasisha matumizi sahihi ya mitandao akiamini itasaidia kujenga na kuruhusu hoja zijibiwe kwa hoja na kufikisha habari kwa jamii bila kudhihakiwa.
Ikumbukwe kuwa, Dorice Mgetta ni mjasiriamali anayejishughulisha na kilimo na ufugaji.

Pia huhamasisha na kusaidia makundi ya vijana na wanawake katika kushiriki shughuli za kujiingizia vipato na kujenga uchumi wa nchi.

“Sambamba na hayo, ninao utaalamu wa kuandaa chakula cha mifugo ninayoifuga kama sehemu ya shughuli zangu za kiuchumi,” anasema.

Uwakilishi wa nchi Kimataifa

“Ndani ya CCM huwa tunasema kila mwanachama mwenye sifa za kuchagulika ni Kiongozi wa akiba, hivyo basi, Dorice Mgetta Kama kiongozi ameshiriki makongamano ya midahalo la kisiasa na kambi nchini UGANDA, liitwalo PYPA, iliyo unganisha vijana wote kwenye siasa Africa mashariki kukiwakilisha chama cha mapinduzi CCM.

“Pia ameshiriki ya kuiwakilisha nchi nchi yetu huko nchini Cameron kwenye kongamano la kuchechemua namna wanasiasa wanavyoweza kushirikiana na Asasi/ Azaki za kiraia barani Afrika kwa amani,” anasema Dorice ambaye anaamini kuwa mabadiliko yanaanza na wewe.

Hivyo hakuna shaka kwamba Dorice Mgetta ni mtu sahihi anayestahili kuvaa viatu vya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) kwa kushirikiana na Mwenyekiti atakayechaguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles