24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TWCC yawapa wanawake Simiyu mbinu ufanyaji biashara nje ya nchi

Derick Milton, Simiyu

Chama cha wafanyabishara wanawake Tanzania (TWCC) kimesema kuwa wafanyabishara wengi wanawawake hapa nchini wanashindwa kufanya biashara ya nje ya nchi kutokana na kutokuwa na elimu ya sheria na taratibu zinazotumika kwa Biashara hizo.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Chama hicho Jackline Maleko, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku nne kwa wajasliamali wanawake Mkoa wa Simiyu, inalenga kuwapatia elimu na mbinu za kufanya biashara nje na ndani ya nchi.

Maleko amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakilalamikia uwepo wa kodi nyingi maeneo ya mipakani pindi wanaingiza bidhaa au malighafi kutoka nje ya nchi, jambo ambalo alisema siyo kweli bali wengi wao hajui sheria na taratibu za ufanyaji wa biashara hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa kutokana na hali hiyo Chama hicho kiliandaa mkakati wa kuhakikisha kinazunguka nchi nzima na kukutana na wanawake wajasliamali ili kuwapatia elimu ya ufanyaji bishara hiyo ambapo wamepanga hadi kufikia 2023 kuwafikia wanawake 10,000.

“ Leo tunakutana na wanawake 100 wa mkoa wa Simiyu kutoka kwenye Wilaya zake zote, kupitia mpango mkakati wetu kama TWCC wanawake wengi sasa wameanza kufanya biashara za kuvuka mipaka baada ya kupatiwa elimu hii,” anasema Maleko

Awali akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, aliwataka wanawake kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia asilimia 10 ya halmashuari ili kuweza kujiendeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles