33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TWAWEZA KIKAANGONI

NA EVANS MAGEGE,DAR ES SALAAM


*Watakiwa kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua kutokana na utafiti waliotoa, COSTECH watoa neno

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Twaweza, imejikuta katika wakati mgumu baada ya Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), kuitaka ijieleze kwanini isichukulewe hatua kwa kukiuka sehemu ya 11 ya Mwongozo wa Taifa wa Usajili na Utoaji wa Matokeo ya Tafiti.

Barua ya COSTECH kwenda Twaweza iliyoandikwa Julai 9, mwaka huu na kusainiwa na Mkurugenzi wa tume hiyo, Dk. Amos Nungu, ilisema taasisi hiyo ilikiuka kifungu hicho kupitia utafiti wake wa ‘Sauti za Wananchi’, ambao matokeo yake yalitolewa Julai 5, mwaka huu.

Matokeo ya utafiti huo, yalionyesha umaarufu wa rais, wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na vijiji na vyama vya siasa umeshuka.

Zikiwa zimepita takribani siku sita tangu kutangazwa kwa matokeo ya utafiti huo, jana kwenye mitandao ya kijamii, barua hiyo ya COSTECH kwenda kwa Twaweza ilianza kusambazwa.

MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, ili kujua kama kweli waliandikiwa barua hiyo, simu yake ilipokewa na dada aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake na kukiri kupokea barua hiyo.

Dada huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake akidai si msemaji mkuu wa taasisi hiyo, alisema bosi wake huyo amesafiri, na kwamba kwa sasa wanafanyia kazi barua waliyoandikiwa.

“Uongozi umenipa maelekezo ya kujibu kuhusiana na barua hiyo, kwamba imeishafika na inafanyiwa kazi… Hapa ni Twaweza, lakini mimi si msemaji mkuu, kwahiyo samahani sana kaka, siwezi kulitaja jina langu kwa maana ya kwamba ulinukuu,” alisema dada huyo.

MTANZANIA lilipotaka kujua alikokwenda Eyakuze, dada huyo alijibu kwa kifupi kwamba ieleweke tu kuwa bosi wake amesafiri.

Alipotafutwa Dk. Nungu ili azungumzie barua hiyo, alisema hawezi kuthibitisha kama ni kweli ni yake na kwamba amewaagiza wasaidizi wake wanachunguza uhalali wake. Hata hivyo, alikiri kuiandikia barua taasisi hiyo.

“Kawaida kwa taasisi zote huwa tunawasiliana kwa njia ya barua na si kwa mitandao ya kijamii, ndiyo maana nimekwambia kwamba wasaidizi wangu wanaichunguza barua hiyo iliyosambazawa, kisha nitatolea ufafanuzi kesho (leo),” alisema Dk. Nungu.

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles