27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Twaha Kiduku alivyomaliza ubabe wa Dulla Mbabe

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Hatimaye gari aina ya Crown lililopewa jina la ‘Crown Mtoa Roho’ limekwenda Morogoro baada ya bondia Twaha Kassim’ Kiduku’ kufanikiwa kumchapa Abdallah Pazi maarufu Dulla Mbabe kwa pointi.

Pambano hilo raundi 10, uzito wa Super Middle, lilifanyika usiku wa kuamkia leo, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Katika pambano hilo, aliyeanza kupanda ulingoni ni Twaha Kiduku aliyesimama kona nyekundu, dakika mbili baadaye akapanda Dulla Mbabe kona ya Bluu na ngumi kuanza kurushwa saa 6:24.

Kila bondia alipanda ulingoni akisindikizwa na wimbo ambapo Twaha Kiduku, aliingia na wimbo wa Bill Nasi unaitwa Mafioso, huku Dulla Mbabe akiingiana na wimbo wa asili ya Kizaramo.

Mashabiki wa Twaha Kiduku hawakuamini kilichotokea raundi ya kwanza katika pambano hilo la raundi 10 baada ya bondia wao kupigwa ngumi moja iliyomkalisha chini.

Kitendo hicho ni kama kilichochea moto kwa Kiduku kwani baada ya kuamka, Dulla Mbabe alipotea karibia raundi nane akichezea kichapo, hali iliyoamsha shangwe kwa mashabiki wa Kiduku wengi wakiwa ni wakazi wa mkoani Morogoro.

Akisimulia hali ilivyokuwa, Kiduku amesema hakujua kama alidondoka ulingoni hadi kocha wake alipomuambia.

“Kwa kweli nilikuwa sijui kama nilidondoka, aliniambia kocha kuwa ulidondoka, nikamuambia mimi napigana au naota, akaniambia pigana mwanangu pigana nikamwambia kocha nashukuru,” amesema Kidukua.

Miongoni mwa mashabiki wa Kiduku walioshudia pambano hilo ni kocha na mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, wanamuziki Afande Sele na Belle 9. Wengine ni Mbunge wa Babu Tale, aliyekuwa mbunge wa Mikumi ambaye mwanamuzi Profesa Jay.

Pambano hilo pia limeshuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.
Katika pambano lingine, Selemani Kidunda alimdunda Paul Kamata raundi ya saba kwenye pambano la raundi 10 na kutwaa ubingwa PST Super Middleweight.

Cosmas Cheka na Ismail Galiatano, walitoka sare baada ya mwamuzi Emmanuel Mlundwa kuvunja pambano kutokana na sababu za kiufundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles