TV za Sony Bravia kuathiriwa na mabadiliko ya Youtube

0
1165

sony-bravia-tv

Runinga za Sony Bravia zilizotengezwa mwaka 2012 hazitoweza kuonyesha tena kanda za video za YouTube baada ya Septemba 30.

Vifaa hivyo havitoweza kuonyesha kanda za video kutoka kwa mtandao huo kutokana na mabadiliko yaliofanywa na You Tube kuhusu vile inavyofanya upakiaji wa video.

Kutokana na hatua hiyo programu ya You Tube katika runinga hizo itaondolewa kufikia mwisho wa mwezi huu, Sony imesema.

Kampuni ya Sony imetoa orodha ya mifano 50 ya runinga ambazo zitaathiriwa na mabadiliko hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here