TUZO SAFI ILA HAYA MUHIMU

0
471

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


SHUGULI ya utoaji tuzo kwa wachezaji waliofanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 ulifanyika Jumatano iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kushirikisha wadau na viongozi mbalimbali wa michezo hususan soka hapa nchini.

Mchakato wa tuzo hizo uliweza kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini wakuu wa ligi, kampuni ya simu za mkononi Vodacom.

Zoezi la upigaji kura liliwahusisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, viongozi wa klabu za ligi na viongozi wa TFF.

Matarajio ya wengi yalikuwa ni kushuhudia washindi wote waliopatikana wakikabidhiwa zawadi zao na kushukuru kwa kuchaguliwa, licha ya kuwa mwaka huu tuzo hizo zimeweza kupiga hatua ila bado mapangufu mbalimbali yameweza kujitokeza na yanahitaji maboresho.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye matamanio ya kufika mbali kisoka na hata maendeleo ya mchezo huo, lazima mabadiliko yaweze kufanyika ili kufanikisha ndoto hizo.

Licha ya kufana kwa tuzo hizo, bado kumeonekana kwua na dosari, baada ya klabu ya Simba kushindwa kutokea wala kutuma muwakilishi.

Simba imeweza kuonyesha kitendo cha fedhea, kwa TFF na kuzihirisha jinsi gani haieshimu viongozi wake wa soka hapa nchini.

Vema kama kutaweza kupatikana sheria itakayowalazimisha wale wote waliochagulia kuwania tuzo na kuwepo kwenye orodha  ya washindani kuwepo siku husika ya tukio.

Endapo suala hili lililojitokeza wakati huu litafumbiwa macho, itafika siku linaweza kufanywa na timu zaidi ya nne na kupelekea tuzo hizo zinakosa wahusika.

Vipengele 11 vilivyoweza kutolewa tuzo

i.Mchezaji bora wa msimu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’(Simba) alifanikiwa kuibuka mshindi na kuwashinda Aishi Manula (Azam), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba) na Haruna Niyonzima( Yanga).

ii.Mchezaji bora wa kigeni, Haruna Niyonzima mchezaji kutoka Rwanda akiwa na aichezea klabu ya Yanga aliweza kuibuka mshindi na kuwabwaga Method Mwanjali (Simba) na kiungo Mrundi wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana.

iii.Kipa Bora Aishi Manula wa Azam FC aliweza kuchukua tuzo hiyo kwa kuwashinda Owen Chaina (Mbeya City) na Juma Kaseja (Kagera Sugar)

iv.Mfungaji Bora tuzo hii iliweza kutolewa kwa watu wachezaji wawili, ambao ni Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), baada ya wote kufunga mabao 14 kila mmoja.
v. Mchezaji bora chipukizi alikuwa ni Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) akiwabwaga  Shaaban Iddi (Azam FC) na Mohammed Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar).

vi. Kocha bora tuzo hii imemuendea Mecky Mexime wa Kagera Sugar, ambaye aliweza kuwashinda  makocha wa kigeni, Mcameroon wa Simba, Joseph Omog na Ettiene Ndayiragije wa Mbao FC.
vii. Mchezaji Bora wa U-20 ni Shaaban Iddi(Azam) ambaye alimshinda mchezaji mwenzake wa timu hiyo Abdallah Masoud ‘Cabaye’ na  Mosses Kitambi(Simba), ambapo tuzo hiyo mwaka huu iliweza kujulikana kama tuzo ya Ismail Khalfan

viii.Bao bora liliweza kuchaguliwa la  Shiza Kichuya, ambaye alilifunga katika mechi dhidi ya Yanga  na kuiwezesha timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo kuwashinda wapinzani wake Peter Mwalyanzi (African Lyon) na Zahoro Pazi (Mbeya City). 
 

viiii. Mwamuzi bora aliweza kuibuka Elly Sasii wa Dar es Salaam, aliyewashinda Shomari Lawi wa Kigoma na Hance Mabena wa Tanga.

ix.Tuzo ya heshima iliweza kumuendea Kitwana Manara aliyeanza, aliyewahi kuzichezea timu za Yanga na Taifa Stars kwa mafanikio.

ixx.Timu yenye nidhamu iliweza kuibuka Mwadui FC ambayo ilipanda daraja misimu miwili iliyopita.

Maboresho tuzo zijayo

Umuhimu wa kuandaliwa kwa sauti na video zinazoonyesha wachezaji husika, wakishukuru kabla na baada ya tuzo hizo kunaweza kuboresha na kuongeza hadhi ya tuzo, pia kutasaidia kuondoa shida ya ukimya pindi mchezaji anaposhindwa kufika eneo la tukio.

Mfano ni kukosekana kwa Tshabalala ambaye tuzo yake ndiyo iliyoweza kubeba dhamana nzima ya michuano hiyo.

Tuzidi kujifunza kutoka kwa wenzetu waliopiga hatua zaidi, ambapo nchi za Ulaya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii ujulikanao kama Sykpe kufanya mahojiano mubashara ‘live’ na mchezaji husika kama ameshindwa kutokea katika tuzo, jambo hilo limekuwa likionekana mara nyingi likifanyika na kwa asilimia kubwa limeweza kujenga heshima ya tuzo mbalimbali duniani.

Imekuwa ikishuhudiwa mchezaji akitafutwa kupitia mtandao huo na kuzungumza moja kwa moja na mashabiki, wadau na wageni walioweza kuhudhuria shuguli husika.

Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC, Saad Kawemba tuzo za mwaka huu zimeonekana  kuboreshwa tofauti na ilivyokuwa misimu ya nyuma, kuanzia kwenye zoezi zima la uteuzi wa washiriki.

Kawemba anasema licha ya kuwepo kwa mapungufu, hususani  upande wa uchaguaji wa mchezaji bora, kwani bodi ya ligi ilitoa orodha ya majina na kutaka yapigiwe kura bila kuweka vigezo vinavyotakiwa kutumika.

“Mchezaji bora wa msimu ndiye anayebeba dhima nzima ya msimu na mashindano kwa ujumla, hivyo ingetakiwa vigezo vya kumpigia kura viwekwe wazi,”anasema Kawemba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here