FARAJA MASINDE
KATIKA Ripoti ya Haki za Binadamu na Bishara Tanzania Bara ya mwaka 2018/19 imeonyesha kuwa bado kuna kiwango kikubwa cha ajira kwa watotosanjari na utumikishwaji wa lazima.
Sote tunajua na kutambua kuwa, Ajira kwa watoto inakatazwa katika mikataba mbalimbali, ikiwamo mkataba wa Kimataifa wa Haki ya za Mtoto(CRC) wa mwaka 1989 na mkataba wa Afrika wa Haki na ustawi wa Mtoto wa mwaka 1990.
Lakaini kama hiyo haitoshi, kazi za lazima pia zinakatazwa katika mikataba mbalimbali, ikiwamo Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani ILO wa kuondoa kazi za za lazima wa mwaka 1957.
Katika ngazi ya taifa, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 inakataza ajira kwa watoto na kazi ya lazima, kwa mujibu wa hii, ‘Mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 hairuhusiwi kuajiriwa kwenye mgodi, kiwanda au kufanya kazi katika sehemu nyingine za kazi ikijumuisha ajira isiyo maalumu na kilimo kwenye mazingira ya kazi ambayo Waziri anaweza kuona ni hatarishi’ hii ni katika kifungu cha 5(3).
Kwani kwa upande wa ajira kwa watoto na kazi ya lazima, ripoti hiyo imeonyesha kuibua mambo makuba mbalimbali katikia mikoa 15 iliyohusishwa na utafiti huo.
Ripoti imeonyesha kuwa matukio ya ajira kwa watoto yaliripotiwa katika mikoa yote iliyofikiwa, lakini jambo hilo liliainishwa kuwa tatizo sugu hasa katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Geita.
Kwani kwa upande wa kulazimishwa kufanya kazi, washiriki katika karibia mahala pote pa kazi walisema kuwa hilo siyo tatizo kwao, japo mtazamo huu nunaweza kuwa umechangiwa na uelewa mdogo kuhusu haki za wafanyakazi na viwango vya kazi.
Hiyo ni kwa uchahe tu katika ripoti hiyo ambayo inaonyesha kuwa watoto wengi bado wako kwenye mnyororo w akutumikishwa ilihali kwamba wako katika umri mdogo ambao kwa namna yoyote walistahili kuwapo shule katika ngazi mbalimbali.
Hata hivyo masuala haya ya watoto kutumishwa yanelezwea kuchangiwa zaidi na kuteteka kw amalezi yanayotolewa na wazazi jambo ambalo limefanya ndoto za watoto wengi kupotea.
Kwa ripoti hii itoshe tu kuwakumbusha wazazi, jamii katika kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao kwa watoto ili kuepusha janga hili la watoto kukacha masomo na kwenda kujiingiza kwenye ajira ilihali kwamba bado siyo umri sahihi.
Hivyo jamii inapswa kuhakikisha kuwa inakuwa mshtari wa mbele katika kukomesha ajira hizi za watoto ikiwa ni pamoja na waajiri wenyewe wanaotoa ajira kwa watoto hawa kuchukuliwa hatua stahiki ili kuja kuwa na taifa la kesho lenye weledi. Ni wajibu wa wazazi na seriakali kuhakikisha kuwa inakomesha mwendelezo wa ajira hizi kwa watoto hasa katika mikoa yenye madini ambako ndiko kumekuwa kukitajwa kuwa na changamoto zaidi.