27 C
Dar es Salaam
Sunday, February 16, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tuwakatae wanasiasa wachonganishi na wafitinishi- CPA MAKALLA

Na Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuachana na viongozi wenye fitna na wachonganishi kwani wanaleta chuki na uhasama hata pale mazuri yanapofanyika katika jamii.

Maneno hayo yametolewa na katibu wa NEC Itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa ndugu Amos Makalla wakati akizungumza na Wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika Viwanja vya Umoja ni nguvu kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 6 Visiwani Zanzibar.

“Sisi CCM tutetembee kifua mbele kazi ya kuwahudumia Wananchi wale wenzetu ni watu wa vituko ,uongo, fitina na majungu ndo kazi yao sisi tunajukumu na dhamana ya kuwaletea Wananchi maendeleo.

“Nayasema ivi kwasababu wanakuja hapa wanasema mnajenga maghorofa wakati watu wanakufa na njaa na miradi yote sio maendeleo sasa ndo ujue kuna shida na anaetamka hayo ni mtu mzima ndo mana nasema kazi ni kusema uongo na vituko lakini hawo hawo Viongozi ndugu zao wanasoma katika hayo maghorofa na wanapata huduma mbalimbali lakini hawazioni niseme muda wa kudanganyana umeisha pamoja majukumu walilojipa tuwaogope Viongozi fitina”

Mwenezi Makalla ameendelea kusema kuwa Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi hawana ubaguzi wowote kwenye suala la kuwaletea maendeleo lakini wenzetu kila kukicha wanaweka fitina na hili kazi kwenu Wazinzabar kwa ujumla wakataeni Viongozi hao na wanasiasa hao kwa kuwanyima kura wakati Uchaguzi utakapofika na tuchague chama cha mapinduzi ambacho ndo kina wajibu wa kuyaleta.

Ziara ya CPA. Amos Makalla visiwani Zanzibar ni sehemu ya maandalizi ya chama cha mapinduzi ya kujiandaa na uchaguzi mkuu mwishoni mwaka huu ambao utawezesha watanzania kuchagua viongozi akiwamo Rais wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles