25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

TUUNGANE KUKUMBATIA UBUNIFU UNAOFANYWA NA VIJANA WA TANZANIA

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKA siku za hivi karibuni tumeshuhudia vijana wa Tanzania wakijikita katika shughuli za kibunifu, hasa wakilenga kutatua changamoto zilizoikumbuka tasnia ya burudani.

Kuna imani mbaya imejengeka kwenye jamii yetu ya kuamini zaidi ubunifu unaofanywa na watu kutoka nje ya nchi hasa Marekani na Ulaya na kudharau kazi za kibunifu zilizofanywa na Watanzania.

Tabia hii inapatikana Tanzania pekee, ni tabia ya ajabu sana na licha ya uajabu wake imeendelea kushika kasi kwenye mitaa hali inayowapa changamoto vijana wabunifu.

Tujifunze kupitia mifano ya wenzetu. Afrika Kusini wana utaratibu wa kucheza nyimbo za wasanii wao kwa 90% huku 10% zikitolewa kwa wasanii kutoka nje ya nchi hiyo.

Nigeria pia wana utaratibu huo, wanakumbatia vitu vyao zaidi kuliko vya wengine, ndiyo maana wametuacha kwenye mambo mengi ya kiburudani sababu sisi tunafanya kinyume kwa kutoa nafasi kwa wageni na kupuuza kazi za kibunifu za vijana wetu.

Tukiachana na masuala ya wasanii tuangalie masoko mapya ya kazi za muziki yanavyoendelea kubuniwa na vijana wa Tanzania halafu sisi wenyewe tunarudisha nyuma harakati hizo za kuipa thamani Bongo Fleva.

Inakuwaje pale vijana wa Tanzania wanapoamua kuwa wabunifu wa kwanza kugundua soko la video ili Serikali inufaike kupitia kodi, hali kadhalika wasanii wafaidike halafu linaibuka kundi la watu wachache wanahujumu ubunifu huo kiasi cha kupoteza mapato ya Serikali na kuwakosesha fedha wasanii.

Inakera sana hii, tumezoea kuona wasanii wakiweka video zao kwenye Youtube na mashabiki hutazama bure kitu ambacho kwa miaka mingi kimepoteza mapato, ikumbukwe kuwa muziki ni huduma na unapaswa kununuliwa kama zilivyo huduma nyingine, iweje sasa tusiunge mkono ubunifu huu?

Hujuma hizo zilifanyika kwenye duka la kimtandao la mkito ambalo huuza audio na hivi sasa limehamia kwenye soko la kimtandao la Afro Premiere ambayo ni kazi ya kibunifu iliyofanyika kuuza video za Bongo Fleva.

Fredy Mgimba, ambaye ni moja ya vijana walioshiriki kubuni soko hilo, anasema kwa wiki mbili tu ambazo wasanii G Nako & Jux na Baghdad & Roma wameweka video   zao sokoni tayari wamepoteza shilingi milioni 30, kutokana na hujuma za watu kuiba video kwenye tovuti hiyo na kuzitundika bure YouTube.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles