28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tutaifanya Wizara hii kuwa mwanga wa Maendeleo ya Jamii-Dk. Gwajima

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima ameitambulisha rasmi Wizara yake kwa Umma na kuwahakikishia kuwa itafanyika kuwa mwanga katika kuongeza kasi kwenye Maendeleo ya Jamii.

Waziri Dk. Gwajima ameyasema hayo leo Januari 17, 2022 jijini Dodoma kwenye Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali, Mtumba wakati akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo katika kikao cha kwanza kukutana tangu kuanzishwa kwa Wizara hiyo Mpya.

Amesema kuwa Wizara ipo tayari kutekeleza majukumu yake sambamba na maagizo mbalimbali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika kufikia azma yake ya kuwaletea wananchi Maendeleo.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu wa kuwepo kwa Wizara ili iweze kuratibu na kuhakikisha wananchi wa makundi yote wanashiriki kusukuma maendeleo ya Taifa lao Sekta zote,” amesema Dk. Gwajima.

Waziri Dk. Gwajima ameongeza kuwa Wizara yake itashirikiana na wananchi na wadau wote katika kuhakikisha kuwa inakuwa kiungo katika kuhakikisha Jamii inakuwa na maendeleo na Ustawi.

Hatua hii inakuja mara baada ya Rais Samia kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum yenye lengo la kuhakikisha jamii inapata Maendeleo na Ustawi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles