22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tutaendelea kuimarisha ushirikiano na AU-Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono na kuimarisha ushirikiano uliopo na Umoja wa Afrika hasa katika kuzingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria.

Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 28, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Mkutano huo unafanyika jijini Arusha.

Majaliwa amesema kwama Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapokea na kushirikiana nao pale watakapohitaji ushauri wa aina yoyote. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo.

Amesema Mahakama hiyo ilianzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kusimamia haki za binadamu, ambapo kwa niaba ya Rais Samia alipata fursa ya kueleza dhamira ya Tanzania katika kuunga mkono jitihada za mahakama hiyo kufanya kazi.

Naye, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo akizungumzia kuhusu ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika inayolenga kulifanya Bara la Afrika kuwa bara lenye nguvu duniani katika siku zijazo amesema kuwa ipo haja ya kutambua changamoto zinazokabili Bara la Afrika ili waifikie Afrika wanayoitaka.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuangalia namna ya kutafsri yote yaliyoanishwa kwenye agenda 2063.

“Lazima tutumie fursa na taasisi zote tulizonazo ili tuweze kufikia Afrika tunayoitaka lengo ni kuhakikisha tunaona maisha ya Waafrika yanaboreshwa na uchumi unakua,” amesema.

Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wanaoupata ambapo unawawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles