25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

TUNDU LISSU AMLIZA WEMA SEPETU

TUKIO la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma juzi, limewagusa watu wengi akiwemo staa wa filamu za kitanzania, Wema Sepetu ambaye ameamua kutumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha hisia zake.

Wema aliandika maneno mengi yenye hisia huku akionyesha kuchukizwa na kitendo hicho ambapo amewataka Watanzania kuendelea kumwombea, mwanasiasa na mwanasheria huyo wa Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) ili Mungu ampe nafuu na arejee kwenye majukumu yake.

“Jamani kwa hili tuombe tu Mungu huyu baba apone… Nikimaanisha, huko alipo sasa Mungu amsimamie na arudi kwenye hali yake, hii sasa imekuwa too much… This is something no one can take… sidhani kama kuna Mtanzania yoyote anayependa hali hii, ni nini hiki jamani…??? Oh Lord help my Uncle… If anything happens to him then nadhani wengi wetu vitatutokea maana hatutokaa KIMYA,” aliandika Wema Sepetu akimlilia Tundu Lissu.

Mastaa wengine walioguswa na tukio hilo Diamond Platnumz, Riyama Ally, Z Anto, Chemical, Roma, Jux, Aunt Ezekiel, Shilole na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,710FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles