27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TUNDA LA KARAKARA SI ZURI KWA WAJAWAZITO, WATOTO

Na HERIETH FAUSTINE,

KARAKARA (Passion) ni tunda linaloota katika mmea unaotambaa ambao wakati mwingine husaidiwa kwa kuweka mti ili uweze kutambaa vizuri na kutoa matunda mengi.

Asili ya tunda hili ni Amerika ya Kusini ambapo inaaminika kuwa kwa mara ya kwanza mmea wake ulipandwa nchini Hawaii, mwaka 1880.

Kwa hapa Tanzania, matunda ya karakara hulimwa zaidi katika  mikoa ya Morogoro, Kigoma, Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Pwani na visiwani Zanzibar.
Kama yalivyo matunda mengine, karakara ni miongoni mwa matunda yaliyo na virutubisho vingi katika mwili wa binadamu.

Virutubisho hivyo ni pamoja na vitamin A, C, B2, B6, na E, flavonoids, pamoja na madini ya chuma. 
Pia ni tunda lililo na uwezo mzuri wa kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na tumbo la hedhi kwa akina mama. 

Tunda hili husaidia kutibu matatizo ya wasiwasi, msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.

Pia husaidia kuboresha afya ya mifupa kutokana na ndani ya tunda hilo kuwapo kwa madini ya  magnesium, copper, phosphorus.

Kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la U.T.I anashuriwa kutumia tunda hili mara kwa mara kwani husaidia kuondoa tatizo hilo.

Ulaji wa matunda ya karakara mawili au matatu kwa siku pamoja na nyama zake za ndani husaidia kuupa mwili nyuzi nyuzi (fibre), Calcium na vilainishi muhimu ambavyo husaidia kuondokana na tatizo la kutopata choo (Constipation).

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili.

Hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanao uwezo wa kusababisha uchungu hivyo kujikuta wakijifungua kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kwao kulitumia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles