30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tunataka Kongwa ya kijani-DC Kongwa

Na Ramadhan Hassan, Kongwa

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk. Selemani Serera amewaongoza wakazi wa Wilaya ya Kongwa kupanda miti zaidi 5000 kandokando ya barabara ya Mbande-Kongwa kwa lengo la kutunza mazingira katika Wilaya hiyo.

Akizungumza leo, Desemba 9, jijini Dodoma, wakati wa zoezi hilo, Dk. Serera ambaye alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa, Dk.Omari Nkullo na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo amesema miti hiyo iliyopandwa ni lazima itunzwe ili iote na kuifanya Kongwa kuwa ya kijani.

Zoezi hilo pia lilifanywa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na Wananchi wa Kongwa.

“Kupanda miti ni jambo moja na kuitunza ni jambo lingine nawaomba sana muitunze miti hii, maana hapa tumepanda na mikorosho kwani katika eneo letu inastawi. Hapa sihitaji kuona mti unekufa nataka istawi na kuota yote,”amesema.

Pia,amesema Wafugaji ni lazima waangalie mifugo yao ili isile miti hiyo kwani katika baadhi ya maeneo Mifugo imekuwa ni changamoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kongwa,Dk.Nkullo amesema wanatekeleza kwa vitendo agizo la Makamu wa Rais la kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka.

Amesema wamepanda miti hiyo kwa km 37 pembezoni mwa barabara ya Kongwa-Mbande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles