23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

“Tumia ulichonacho kuleta mabadiliko kwa mtoto wa Tanzania”-Repssi

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Jamii imekumbushwa umuhimu wa kuwahudumia watoto ili kuwaepusha na msongo wa mawazo unaopelekea kuathirika kisaikolojia na kuharibu ndoto zao.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Oktoba 13, 2021 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Repssi Tanzania, Jeanne Ndyetabura wakati wa Kongamano la sita la Msaada wa Kisaikolojia lililoandaliwa na Shirika la Regional Psychosocial Support Initiative REPSSI.

Sehemu ya washiri wa Kongamano hilo upande wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Kongamano hilo linalofanyika kwa siku tatu kuanzia leo linafanyika Mjini Maputo, Msumbiji ambapo Tanzania inaungana na nchi nyingine 12 kufuatilia kwa njia ya mtandao kutokana na janga la Uviko 19.

Jeanne amesema kuwa kila mtu ana wapaswa kutumia kitu alichonacho ili kuleta mabadiliko kwa watoto wa Tanzania.

“Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua kujiona kuwa ana mchango wa katika kumsaidia mtoto wa Tanzania ili kujenga taifa bora la kesho.

“Kama tunavyojua kwamba zaidi ya nusu ya Watanzania ni watoto, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anamsaidia mtoto mmoja ili aweze kukua kwenye misingi na ustawi kwa manufaa ya kesho.

“Hivyo, ndiyo maana Repssi tumekuwa tukiimiza kila mwaka kuhakikisha kuwa watoto wanajengewa mazingira mazuri ya kisaikolojia kwa kuwa ndio msingi wa kufikia ndoto zao,” amesema Jeanne.

Amesema kwa mwaka huu kongamano hilo litakalodumu kwa siku tatu linabebwa na dhima ya Ubunifu, Jumhishi na Kustawi.

Upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala amesema makuzi ya watoto yanapaswa kutiliwa mkazo hususan afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa ajili ya kuwasaidia kutimiza malengo yao.

“Kumekuwa na changamoto nyingi zinazowakabili watoto lakini kubwa unakuta kwamba kukosekana kwa msaada wa kisaikolojia imekuwa ni moja ya sababu inayochochea watoto wengi kupitia madhila mengi na hata kukatisha ndoto zao,” amesema Mapalala.

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala, akifuatilia mjadala kwenye kongamano hilo linalofanyika kwa njia ya mtandao kutoka Maputo, Msumbiji.

Aidha, Mapalala ameongeza kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zilizowasilishwa na watoto wa Tanzania ni pamoja na janga ka Uviko 19 ambao walikosa msaada wa kisaikolojia na taarifa sahihi.

“Janga la corona lilikuwa ni sehemu ya changamoto kubwa ambayo iliwakabili watoto na jamii kwa ujumla na hata kusababisha ukosefu wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto kwani walikuwa wakipata mkanganyiko wa taarifa na kukosa ipi ni sahihi na ispi ni uzushi.

“Hata hivyo pamoja na mazingira hayo watoto wa Tanzania waliweza kuelezea changamoto zao akiwamo ya kuhitaji kuwapo kwa maofisa ustawi shuleni, pia wameibua changamoto ya usafirishaji wa watoto sambamba na kukosa fursa sawa kwa wale wenye ulemavu hasa kwenye nyanja ya elimu,” amesema Mapalala.

Amesema mwaka huu mkutano huo unafanyika nchini Msumbiji lakini kutokana na changamoto ya Uviko -19 unafanyika kwa njia ya mtandao huku idadi ndogo tu ya washiriki ndio wakiwakilisha nchini Msumbiji.

Upande wake, Cecilia Kaduga amesema wao kama watoto wa Tanzania moja ya changamoto wanazokutana nazo ni mimba na utumikishwaji katika umri mdogo na kutokuwa na haki ya kujieleza wakasikilizwa.

“Hivyo maombi yetu kwa Serikali ili kuweza kukabiliana na baadhi ya changamoto kwa watoto ni uwepo wa maofisa ustawi shuleni ili waweze kuwa msaada kwetu,” amesema Cecilia.

Repssi ni Shirika lisilolakiserikali linalojihusisha na utoaji wa huduma ya Afya ya Akili na Msaada wa kisaikolojia likiwa katika nchini 13 za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles