29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Tume yabaini kukosekana mkakati wa kuzuia uhalifu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Tume ya Kurekebisha Mifumo ya Haki ya Jinai, imesema kwenye tathimini yao wameona vyombo vingi vya haki jinai vinatumia nguvu kubwa kupambana na uhalifu na kugundua nchi haina mkakati wakubaini na kuzuia uhalifu .

Hayo yamebainishwa leo Novemba 8,2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande alipokutana na mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchi na taasisi zao nchini na kuwapa mrejeshi wa taarifa ya tume ya kuboresha miundo ya taasisi za haki jinai.

Amesema amewahakikishia mabalozi na wawakilishi hao kuwa baadhi ya mapendekezo yaliyowasilishwa na tume hiyo yameanza kufanyiwa kazi na Serikali.

“Tukasema hapana hiyo ni nzuri sawa lakini lazima tujikite kubaini na kuzuia uhalifu siyo unangoja utendeke alafu unapambana nao,” amesema Jaji Chande.

Amesema jambo moja limejitokeza, kuangalia je wajikite kwenye kupambana na uhalifu au kubaini na kuzuia uhalifu? hivyo moja ya mapendekezo yao kwenye hizo taasisi kubwa za haki jinai zibadilishe usukani zijikite kwenye kubaini na kuzuia uhalifu .

Ametaja baadhi ya mapendekezo yaliyoanza kutekelezwa ni pamoja na kufunguliwa kwa ofisi 50 za mkurugenzi wa mashitaka katika ngazi ya wilaya nchini ili kusaidia upatikanaji wa haki nchini ikiwa ni moja ya mapendekezo ya kuboresha mfumo wa haki jinai.

Amesema kufunguliwa kwa ofisi hizo za mashitaka katika wilaya 50 nchini ni jambo lililopendekezwa na tume tangu awali.

Aidha Jaji Chande amesema wamebaini hawana sera ya Taifa ya haki jinai hilo ni jambo ambalo wametoa mapendekezo yao kwenye ripoti zao zaidi ya 360, taasisi zibainishe kipaumbele katika yale mapendekezo yanayowahusu wao au yanawahusu wenzao.

Amesema ripoti hiyo ni fursa yao ya pili kwa sababu walivyoteuliwa kama tume na balozi hizo na mabalozi wameona wawapitishie mapendekezo ya tume ili na wao watoe michango yao.

Amesema na wao wametoa michango ikiwemo mabalozi saba akiwemo balozi wa Indonesia ambapo amesema sasa hivi Indonesia na Tanzania wapo katika matayarisho ya ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenda nchini humo na wanategemea kwenye ziara hiyo ushirikiano baina ya Polisi wa Tanzania na Polisi wa Indonesia kuimairishwa.

Akizungumza Katika kikao hicho
Naye kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Balozi wa Visiwa vya Comoro, Dk. Ahamada El Badaoui amesema kazi iliyofanywa na tume ni njema na wao kama mabalozi wanaunga mkono juhudi za serikali katika kutoa haki na kuahidi kuendelea kutoa mchango wao wa ushirikiano na Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Nigeria nchini, Hamisu Umar Takamawa, ameipongeza kamati kwa kufanya kazi ndani ya muda mfupi na kuja na mapendekezo ambayo ni mazuri na kusema Tanzania ikiyatekeleza itapiga hatua zaidi na kusema Nigeria wana cha kujifunza kupitia tume hiyo.

“Tumefarijika na taarifa hii, kwa kweli Nigeria tutakuja kuiga mfano huu wa kutekeleza haki jinai hapa Tanzania,” amesema Balozi Takamawa.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Shalini Bahuguna, ameipongeza tume kwa kuweka mapendekezo ya kuboresha haki za mtoto na kueleza kuwa UNICEF ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuimarishwa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles